• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Huduma

MAENEO YA KIUTAWALA MKOA WA KATAVI

KWA MUJIBU WA MAREKEBISHO YA TANGAZO LA SERIKALI NA. 220 & 221 KWA MAMLAKA ZA MIJI NA WILAYA

S/N

HALMASHAURI

TARAFA

KATA

VIJIJI

VITONGOJI

MITAA

JIMBO

01

MPANDA MC

2 -Kashaulili na Misunkumilo.

15

14

81

43

MPANDA KATI

02

MPANDA DC

3-Karema, Kabungu na Mwese.

16

55

328

-

MPANDA VIJIJINI

03

NSIMBO DC

2-Nsimbo na Ndurumo

12

59

272

-

NSIMBO

04

MLELE DC

1-Inyonga

6

18

85

-

KATAVI

05

MPIMBWE DC

2-Mpimbwe na Mamba

9

31

165

-

KAVUU

JUMLA

10

58

177

931

43

5


 

WILAYA TATU ZA MKOA NA MAENEO YA KIUTAWALA 

S/N
WILAYA
HALMASHAURI
TARAFA
KATA
VIJIJI
VITONGOJI
MITAA
JIMBO

01

MPANDA
NSIMBO DC &
MPANDA MC

4

27

73

353

43

NSIMBO
MPANDA
MJINI

02

TANGANYIKA
MPANDA DC

3

16

55

328

-

MPANDA
VIJIJINI

03

MLELE
MLELE DC
MPIMBWE DC

3

15

49

250

-

KATAVI
KAVUU

JUMLA

5

10

58

177

931

43

5


MGAWANYO WA MAJUKUMU

1.1.1 Mkuu wa Mkoa 

  • Kifungu 61 (4-5) cha Katiba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kifungu cha 5-7 vya Sheria za Tawala za Mikoa Na. 19 ya 1997 Mkuu wa Mkoa atasimamia kazi na shughuli zote za Serikali ya Muungano wa Tanzania katika Mkoa. Sheria husika ni pamoja na:
  • Sheria Na. 19 ya mwaka 1997 ya Uanzishwa ji wa Tawala za Mikoa, Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC)
  • Sheria Na. 24 ya mwaka 1966 ya Ulinzi na Usalama wa Taifa, Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU), Katibu Tawala wa Mkoa atasimamia Maagizo ya KUU.
  • Sheria Na. 16 ya mwaka 1964 ya Utumishi wa Umma, Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi wa vijana Jeshi la Taifa (JKT)
  • Sheria Na. 7 na 8 ya mwaka 1982 ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mkuu wa Mkoa anawajibika kusimamia Halmashauri za Wilaya.
  • Kutoa ushauri wa kitaalam kwa Halmashauri ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

1.1.2 Katibu Tawala wa Mkoa 

  • Katibu Tawala wa Mkoa ana Jukumu la kumshauri Mkuu wa Mkoa na kuwa mtekelezaji Mkuu wa shughuli za uongozi wa Sekretarieti ya Mkoa kulingana na sheria ya Tawala za Mikoa Na. 19 ya 1997. Pia ni mshauri Mkuu wa Mkuu wa Mkoa katika masuala ya sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za Serikali za Mitaa. Aidha Katibu Tawala wa Mkoa anawajibika kwa kwa fedha zote za Sekretarieti ya Mkoa.

Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC)

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) ipo kwa mujibu wa (Kifungu cha 9 cha sheria ya Tawala za Mikoa Na. 19 ya 1997). RCC ni chombo cha kutoa ushauri fasaha utakaomsaidia Mkuu wa Mkoa kutoa miongozo ya utekelezaji Mkoani. Pia ni sehemu pa kujadili mambo yote ya Mkoa na kutoa fursa nzuri zaidi ya kushauriana na kuratibu mipango ya maendeleo na utekelezaji wake.

1.1.3.1 Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa 

  • Mkuu wa Mkoa (Mwenyekiti)
  • Wakuu wa Wilaya
  • Wenyeviti wa Halmashauri
  • Wakurugenzi wa Halmashauri
  • Wabunge wote wa majimbo
  • Wabunge viti maalum wote
  • Katibu Tawala wa Mkoa (Katibu)

1.1.4 Sekretarieti ya Mkoa 

Majukumu ya Msingi ya Sekretarieti ya Mkoa:

  • Sekretarieti ya Mkoa ina wajibu wa kumshauri na kumsaidia Mkuu wa Mkoa kutekeleza majukumu yake, hususan:-
  • Kudumisha Ulinzi na Usalama
  • Kutoa ushauri wa kitaalam kwa Halmashauri ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
  • Sekretarieti ya Mkoa inatoa aina nne za huduma za kuzisaidia Halmashauri kama ifuatavyo:-
  • Huduma za usimamizi wa kazi (management supportive services) katika fani za Serikali za Mitaa, sheria,Uchumi, takwimu, Maendeleo ya jamii na ukaguzi wa hesabu
  • Huduma za Maendeleo ya Kiuchumi (economic development support services) katika fani za kilimo, mifugo, biashara, Maliasilisi na Ushirika.
  • Huduma za Mipango ya ardhi na uhandisi (physical planning and engineering support services) katika fani za uhandisi, mipango miji na upimaji.
  • Huduma za jamii (Social Sector support services) katika fani za Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii na Maji.

1.2 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya 

  • Madaraka yake yanatiririka kutoka kwa Rais kupitia kwa Mkuu wa Mkoa
  • Madaraka kwa mujibu wa sheria Na 19 ya 1997 (kumweka mtu kuzuizini masaa 48 mfulilizo)
  • Sheria Na. 7 ya 1982 kusimamia halmashauri
  • Sheria ya Ndoa Na. 5 ya 1971 kufungisha ndoa (civil marriages) 

1.3 Katibu Tawala wa Wilaya 

Ni mshauri na mtekelezaji Mkuu wa shughuli zote za Serikali katika Wilaya

Kumshauri Mkuu wa Wilaya katika masuala yahusuyo

  1. Ulinzi na Usalama
  2. Utekelezaji wa majukumu ya sherehe na dhifa
  3. Malalamiko ya wananchi
  4. Kuandaa makadirio ya matumizi
  5. Msajili wa ndoa
  6. Kusaidia Halmashauri kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria

1.4 Afisa Tarafa 

  • Ni mshauri na msaidizi wa Mkuu wa Wilaya katika kutekeleza shughuli za Serikali katika eneo la Tarafa yake.
  • Kuhimiza utekelezaji wa Sera za Serikali tarafani
  • Amani na UTULIVU
  • Kuratibu shughuli za maafa na dharura
  • Kushughulikia malalamiko ya wananchi
  • Kusimamia na kuhimiza shughuli za maendeleo

MUUNDO WA SEKRETARIETI

1.

Sehemu ya UTAWALA NA RASILIMALI WATU

2.

Sehemu ya MIPANGO NA URATIBU

3.

Sehemu ya AFYA NA USTAWI WA JAMII

4.

Sehemu ya ELIMU

5.

Sehemu ya UCHUMI NA UZALISHAJI

6.

Sehemu ya MIUNDOMBINU

7.

Sehemu ya MAJI

8.

Sehemu ya MENEJIMENTI YA SERIKALI ZA MITAA

1.

Kitengo cha FEDHA NA UHASIBU

2.

Kitengo cha UKAGUZI WA NDANI

3.

Kitengo cha HUDUMA YA SHERIA

4.

Kitengo cha UNUNUZI NA UGAVI

5.

Kitengo cha HABARI NA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO

2. SEHEMU YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU

LENGO:- Kutoa usaidizi wa utaalam na huduma za utawala na Menejimenti ya Utumishi kwenye Sekretarieti ya Mkoa

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma pamoja na sheria zinazotawala uendeshaji wa Utumishi wa Umma.
  • Kushirikiana na OR-MUU-Sekretarieti ya Ajira katika masuala yote yahusuyo ajira za watumishi.
  • Kutoa huduma za masjala na Utunzaji wa Kumbukumbu.
  • Kutoa huduma za Ki-protokali.
  • Kuratibu huduma za ulinzi, usafi, matengenezo, nyumba na usafiri.
  • Kusimamia masuala yote ya ajira na utumishi wa watumishi (kuthibitisha, kupandisha vyeo, kuendeleza watumishi, mpango wa raslimali watu, upimaji wa Wazi (OPRAS), mishahara na stahiki zinginezo, likizo, hitimisho la ajira, nidhamu malalamiko nk.) katika Sekretarieti ya Mkoa.
  • Kumshauri Katibu Tawala Mkoa kuhusu masuala ya Utawala, Utumishi na raslimali watu.
  • Kusimamia masuala ya nidhamu kwa watumishi.

3. MIPANGO NA URATIBU

LENGO:- Kutoa usaidizi wa utaalam na huduma katika nyanja ya mipango na bajeti

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kuratibu maandalizi, usimamizi na tathmini ya mipango (mpango mkakati, mpango kazi na bajeti)
  • Kuhudumu kama Sektretarieti kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC)
  • Kupitia na kuunganisha maandalizi na utekelezaji wa mipango na bajeti ya mkoa (VOTE 87)
  • Kushauri na kuratibu shughuli za utafiti kwenye Mkoa
  • Kuratibu zoezi la sensa ya watu na makazi
  • Kufuatilia na kutathini utendaji wa Halmashauri / Mamlaka za Serikali za Mitaa
  • Kuratibu menejimenti ya kukabiliana na maafa katika Mkoa
  • Kumshauri RAS juu ya shughuli za mashirika, asasi za kijamii na sekta binafsi

4. SEHEMU YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

LENGO:- Kuwezesha utoaji wa afya ya kinga, tiba, maendeleo ya afya na ustawi wa jamii kwenye Mkoa

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kuratibu na kushauri juu utekelezaji wa sera ya afya kwenye Mkoa
  • Kufuatilia na kuzisimamia watoa huduma za afya zinazotolewa na Serikali na Sekta binafsi
  • Kujengea uwezo MSM katika utoaji wa huduma za afya
  • Kutoa msaada wa kitaalam kipindi cha milipuko ya magonjwa
  • Kutoa ushauri wa kitaalam katika mipango ya kukabiliana na UKIMWI kwenye Mkoa

5. SEHEMU YA ELIMU

LENGO:- Kuwezesha utoaji wa huduma ya elimu pamoja na kusimamia mitihani ya elimu isiyo rasmi elimu ya msingi na sekondari.

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kuratibu utoaji wa elimu ya awali, msingi, sekondari na elimu ya watu wazima
  • Kuratibu utekelezaji wa sera ya elimu na ufundi mkoani na kutoa ushari
  • Kuratibu ukusanyaji, uchakataji na kutafsiri na kusambaza takwimu za elimu na takwimu za elimu ya ufundi katika Mkoa.
  • Kusimamia mitihani ya elimu ya msingi, sekondari na chuo cha walimu katika Mkoa
  • Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa taarifa za kaguzi za shule
  • Kuratibu upangaji wa walimu kwenye shule katika mkoa

6. SEHEMU YA UCHUMI NA UZALISHAJI

LENGO:- Kuwezesha utoaji wa ushauri wa kitaalam katika sekta za uchumi na uzalishaji kwenye Halmashauri.

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kuratibu utekelezaji wa sera ya kilimo, mifugo, uvuvi, ushirika, misitu, viwanda, biashara na masoko katika mkoa
  • Kujengea uwezo MSM kwa kutoa ushuari wa kitaalam katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, biashara na masoko,
  • Kushauri MSM juu uanzishaji wa ushirika na ukaguzi wa vyama vya ushirika na SACCOS
  • Kushauri MSM juu ya maeneo yanayofaa kwa uwekezaji
  • Kusaidia MSM kutekeleza sheria ya hifadhi ya Mazingira (Sheria Na. 2 ya 2004)
  • Kutoa ushauri kwenye masuala ya kilimo cha umwagiliaji

7. SEHEMU YA MIUNDOMBINU

LENGO:- Kuwezesha utoaji wa ushauri wa kitaalam katika maendeleo ya miundombinu kwa Halmashauri

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kuratibu utekelezaji wa shughuli za barabara, majengo, nishati, upimaji, ardhi na mipango miji
  • Kujengea uwezo MSM katika masuala ya ujenzi wa barabara, majengo, nishati, upimaji na mipango miji
  • Kuandaa ramani za mipango miji
  • Kukagua na kushauri juu ya michoro ya kihandisi kwa shughuli zinazotekelezwa kwenye mkoa
  • Kumshauri RAS juu tathmini ya athari ya kimazingira (Environmental Impact Assessment)

7. SEHEMU YA MAJI

LENGO:- Kutoa ushauri wa kitaalam kwa MSM juu ya maendeleo ya sekta ya maji

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kuratibu, kuchambua na kushauri juu ya utekelezaji wa sera ya maji Mkoani
  • Kuzijengea uwezo MSM katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya sekta ya maji
  • Kuzisaidia MSM kuandaa mipango inayotekelezeka ya kuendeleza miundombinu ya maji katika ngazi za Vijiji na maeneo ya miji
  • Kufanya ufuatiliaji wa ujenzi wa miradi ya maji katika MSM kusudi miradi hiyo itekelezwe kwa ubora
  • Kuratibu programu ya usambazaji maji vijijini na usafi wa mazingira

9. SEHEMU YA MENEJIMENTI YA SERIKALI ZA MITAA

LENGO:- Kutoa ushauri wa kiutaalam na huduma kwa MSM ili kuimarisha utawala bora.

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kutoa ushauri juu ya matumizi sahihi ya fedha za umma kwa MSM
  • Kufanya tathmini namna MSM zinavyotekeleza shughuli zake kama zinazingatia sheria, kanuni, taratibu
  • Kuratibu na kushauri MSM juu ya menejimenti ya rasilimali watu (ajira, upangaji vituo, nidhamu na upandishaji vyeo)
  • Kusaidia MSM kuandaa bajeti na matumizi sahihi ya rasilimali fedha
  • Kushauri na kusaidia MSM juu masuala ya kiutawala
  • Kutoa ushauri juu ya marejeo ya miundo ya Halmashauri (LGA structure)

KITENGO CHA FEDHA NA UHASIBU

LENGO:- Kutoa huduma bora ya usimamizi wa fedha na uhasibu

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kuandaa bajeti na kusimamia matumizi
  • Kujibu hoja za ukaguzi kutekeleza ushauri wa Mkaguzi
  • Kutayarisha malipo mbalimbali
  • Kutayarisha taarifa za makato ya kisheria na kuwasilisha kunakohusika

KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI

LENGO:- Kutoa ushauri kwa Afisa Masuhuli juu matumizi sahihi rasilimali fedha kama imefuata miongozo ya matumizi ya fedha za umma

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kukagua na kutoa taarifa juu usimamizi na menejimenti ya rasilimali fedha.
  • Kukagua na kutoa taarifa juu ya matumizi ya fedha kama imezingatia kanuni na sheria ya matumizi ya fedha za umma
  • Kukagua mifumo iliyopo inayotumiwa kutunza rasilimali

KITENGO CHA UGAVI NA UNUNUZI

LENGO:- Kutoa huduma ya ununuzi na ugavi wa vifaa na huduma kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kushauri Menejimenti juu masuala ya ununuzi wa vifaa na huduma
  • Kuandaa mpango wa ununuzi kwa mwaka husika
  • Kutunza na kuhuisha inventory ya vifaa mbalimbali
  • Kuratibu ufutaji wa mali na vifaa visivyotumika

KITENGO CHA TEHAMA

LENGO:- Kuwezesha utoaji wa ushauri wa kitaalam katika sekta za uchumi na uzalishaji kwenye Halmashauri

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kushauri Menejimenti juu ya mausala ya TEHAMA na utekelezaji wa e-government/serikali mtandao
  • Kufuatilia na kusaidia MSM juu ya masuala TEHAMA
  • Kutoa msaada wa kiufundi katika matumizi ya vyombo vya kielektroniki
  • Kushauri Menejimenti juu ya utekelezaji wa sera ya TEHAMA

KITENGO CHA HUDUMA YA SHERIA

LENGO:-Kutoa huduma ya kisheria kwa RS na LGA

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:-

  • Kutoa ushauri wa kisheria na usaidizi kwa RS na MSM juu ya tafsiri ya sheria, mikataba, makubaliano, ushauri wa kitaalam, na kushirikiana mwanasheria wa Serikali.
  • Kushiriki kwenye majadiliano mbalimbali na mikutano yenye kuhitaji usaidizi wa kisheria.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MRINDOKO AZINDUA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU (GAWE) 2025

    May 05, 2025
  • RC MRINDOKO AIHAKIKISHIA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI USALAMA WA UCHAGUZI MKOANI KATAVI.

    April 29, 2025
  • WAZIRI NDEJEMBI AONGOZA MIKAKATI YA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI ENEO LA WESTERN, KITONGOJI CHA LUHAFWE – H/ WILAYA YA TANGANYIKA

    April 24, 2025
  • PPPC WATOA ELIMU UIBUAJI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA UBIA.

    April 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved