Mhe. Salehe Mbwana Muhando
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.Salehe Muhando (wa tatu kutoka kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Ally Hapi
kuhusu Wilaya yake ilivyojipanga kuhakikisha inamnyanyua mkulima kutoka katika kilimo cha kimazoea na kuingia katika kilimo cha kibiashara.
Viongozi hawa wamekutana baada ya kufungwa kwa maonesho ya nanenane mwaka 2018 katika ukumbi wa Benjamini Mkapa Jijini Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Muhando wa pili kutoka kulia akisikiliza maelezo ya maabara ya udongo
inayotembea katika banda la OCP, wakati wa maonesho ya Nane nane Jijini Mbeya mwaka 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Mhando wa kwanza kushoto akiwa katika ziara ya kujifunza teknolojia mpya
inayotumika katika Kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya Chakula na Biashara na kujenga uchumi wa Viwanda katika
maonesho ya Nanenane Jijijini Mbeya 2018. Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
Bw. Lumuli Rojasi na wa tatu ni Mhe. Hamadi Mapengo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Muhando akikagua kitalu cha miche ya Mikahawa na Pines katika
Kijiji cha Lugonesi kata ya Mwese Wilaya ya Tanganyika
Kitalu cha miche ya Mikahawa na Pines katika Kijiji cha Lugonesi kata ya Mwese Wilaya ya Tanganyika
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe.Salehe Muhando akikagua Miradi ya Maendeleo katika Wilaya yake, ili kuhakikisha
kuwa ujenzi unaendana na thamani ya fedha iliyotolewa na kukamilika kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Muhando akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Maji katika Kata ya Kabungu.
Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza wakandarasi wa Mradi huo, na kuwaambia kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo
na kuwataka wakamilishe mradi huo kwa muda uliopangwa.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Mheshimiwa Salehe Mhando amepokea vifaa mbalimbali kutoka NMB
kwa ajili ya kituo cha afya cha Mwese vyenye thamani ya million 5.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Mhando ametoa shilingi milioni moja katika kuunga mkono jitihada za wananchi wa Kijiji
cha Luhafwe ambao wameanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Ruhafwe iliyopo wilayani Tanganyika.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika akiwa katika vikao vyake vya kawaida kuhamasisha wananchi kufanya kazi
na kuwa wabunifu katika kujiongezea kipato na kujenga uchumi wa Viwanda.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh.Salehe Mbwana Mhando akiwa katika ziara ya na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika
Wilaya yake, Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na kutembelea miradi ya ujenzi katika Kata ya Ikola pia alipata fursa ya kutembelea
Mwalo katika eneo la Kata ya Ikola na kuwahimiza wavuvi kufanya kazi kwa bidii ili kuijenga Tanzania mpya ya Viwanda.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved