Bw. Godfrey Mallembo
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Mkoa
Lengo kuu la Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani katika Sekretarieti yaMkoa wa Katavi ni kutoa ushauri kwa Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoajuu ya matumizi sahihi ya rasilimali fedha kama imefuata sheria, kanuni namiongozo ya matumizi ya fedha za umma.
Kitengocha Ukaguzi wa Ndani kinahusika katika kukagua mifumo mbalimbali iliyowekwa ilikutumika kutunza rasilimali mbalimbali za Serikali kama inatumika ipasavyo nakufuatwa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kulingana na mifumo hiyo.
PiaKitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinahusika katika usimamizi wa thamani ya fedha(Value for Money) katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na kusimamiwa naSekretarieti ya Mkoa wa Katavi. Kitengo kinakagua na kuhakiki mradi kamaunaendana na thamani halisi ya kiwango cha fedha kilichotumika.
KatikaSekretarieti ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kina watumishi wawili wanaofanyakazi ya Ukaguzi wa ndani Katika Sekretarieti ya Mkoa wa Katavi, pamoja na Ofisiza Wakuu wa Wilaya za Mlele, Mpanda na Tanganyika.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved