• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

TIMU YA WATAALAMU WA ELIMU KUTOKA ZANZIBAR YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO H/W YA MPIMBWE.

Posted on: February 4th, 2026

Katika juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma na kubadilishana uzoefu katika sekta ya elimu, timu ya wataalamu wa elimu kutoka Zanzibar imeendelea na ziara yao ya siku tano ya mafunzo mkoani Katavi kwa kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Februari 04, 2026.

Ziara hiyo imelenga kujifunza na kushirikishana mbinu bora za utekelezaji wa sera na mipango ya elimu, hususan katika maeneo ya elimu ya awali, msingi na sekondari, pamoja na matumizi ya teknolojia na rasilimali rafiki kwa mazingira.

Akiwa wilayani Mpimbwe, ujumbe huo umetembelea Shule ya Sekondari Mizengo Pinda ambako umejifunza kuhusu matumizi ya mfumo wa nishati safi ya kupikia, hatua inayolenga kupunguza matumizi ya kuni na mkaa pamoja na kulinda mazingira. Aidha, wataalamu hao walipata fursa ya kutembelea darasa la awali pamoja na Shule ya Msingi Ibuka, ambapo walijionea mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji pamoja na juhudi zinazochukuliwa kuboresha elimu ya msingi.

Ziara hiyo pia ilihusisha kutembelea chemchemi ya maji ya moto, kama kivutio cha asili na rasilimali ya kipekee ya Halmashauri hiyo, pamoja na kiwanda cha kuchakata mchele, ambapo ujumbe huo ulipata maelezo kuhusu mchango wa sekta ya kilimo na viwanda vidogo katika kuinua uchumi wa wananchi na kusaidia maendeleo ya elimu kupitia mapato ya ndani.

Kwa ujumla, ziara hiyo imeelezwa kuwa na manufaa makubwa kwa pande zote mbili, ambapo wataalamu kutoka Zanzibar wamepata uzoefu wa vitendo, huku Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ikiendelea kujitangaza kama kitovu cha ubunifu na ushirikiano katika sekta ya elimu na maendeleo ya jamii.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • RATIBA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI - MWAKA 2025 April 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOA WA KATAVI August 27, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOA WA KATAVI August 27, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATAALAMU WA ELIMU KUTOKA ZANZIBAR WAVIKA H/W YA MLELE KUJIFUNZA.

    February 05, 2026
  • TIMU YA WATAALAMU WA ELIMU KUTOKA ZANZIBAR YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO H/W YA MPIMBWE.

    February 04, 2026
  • MHE. WAZIRI DKT. HOMERA ASISITIZA HUDUMA ZA KISHERIA NA UWAJIBIKAJI, VIONGOZI MKOA WA KATAVI WAPONGEZWA

    February 11, 2026
  • RAS MSOVELA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA WILAYA YA TANGANYIKA KUWA MFANO WA KUIGWA, KUJENGA HUDUMA BORA, UWAZI NA UWAJIBIKAJI.

    December 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved