Bi. NEWAHO E. MKISI
Katibu Tawala Msaidizi
Sehemu ya Elimu.
1.0 SEHEMU YA ELIMU
1.1 UTANGULIZI
Sehemu ya Elimu ni moja ya Sehemu zinazounda Sekretarieti ya Mkoa wa Katavi. Jukumu kubwa la Sehemu hii ni Kufafanua na Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari, Mafunzo ya Ualimu, Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi na Vituo vya Ufundi Stadi katika Mkoa wa Katavi.
1.2 MUUNDO WA SEHEMU
Kimuundo Sehemu hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi.
Watumishi waliopo katika Sehemu hii.
NA |
JINA |
CHEO |
1 |
Newaho E. Mkisi
|
Katibu Tawala Msaidizi – Elimu
|
2 |
Florence Ngua
|
Afisa Elimu Taaluma - Msingi
|
3 |
Wilson M. Berthord
|
Afisa Elimu Taaluma - Sekondari
|
4 |
Beatrice C. Gati
|
Kaimu Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi
|
Aidha Kimuundo Sehemu hii inatakiwa kuwa na Jumla ya Watumishi Saba (7) Wafuatao, Ikionyesha Waliopo na Pungufu yao.
NA. |
CHEO/KADA |
MAHITAJI |
WALIOPO |
PUNGUFU |
1. |
Katibu Tawala Msaidizi (Afisa Elimu Mkoa)
|
1 |
1 |
0 |
2. |
Afisa Elimu Taaluma Mkoa
|
3 |
2 |
1 |
3. |
Afisa Elimu Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi
|
1 |
1 |
0 |
4. |
Afisa Michezo
|
1 |
0 |
1 |
5 |
Afisa Vijana
|
1 |
0 |
1 |
|
JUMLA
|
7 |
4 |
3 |
MAJUKUMU YA SEHEMU YA ELIMU
Kushughulikia upanuzi wa Elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Ufundi, Elimu ya Watu Wazima, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu
Kuratibu, kusimamia, kuendesha na kutathmini Mitihani ya Darasa la Nne na Saba, Kidato cha Nne na Sita, Mafunzo ya Ualimu pamoja na Mitihani ya Ufundi katika Mkoa kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Tanzania, OR-TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za Wathibiti Ubora wa Shule
Kusimamia utekelezaji wa kazi za Maafisa Elimu wa Halmashauri waliopo katika Mkoa
Kuratibu na kuchambua takwimu za Elimu katika Mkoa kwa ajili ya Mipango ya maendeleo katika ngazi za Halmashauri na Taifa
Kusimamia na kuendesha uchaguzi wa Wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Kwanza katika Mkoa
Kuratibu na kusimamia uhamisho wa wanafunzi wa Elimu ya Msingi na Sekondari ndani na nje ya Mkoa
Kuratibu, kusimamia na kuendesha mashindano ya Taaluma katika ngazi ya Mkoa
1.4 MGAWANYO WA KAZI NA SHUGHULI KATIKA SEHEMU YA ELIMU
NA |
JINA |
CHEO |
MAJUKUMU |
1. |
Newaho Mkisi
|
Mkuu wa Sehemu ya Elimu (Afisa Elimu Mkoa)
|
Anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa juu ya utendaji wa shughuli zote za Sehemu.
Kuhudhuria vikao vyao vya kisheria anavyotakiwa kuhudhuria Kushughulikia upanuzi wa Elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Ufundi, Elimu ya Watu Wazima, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu Kuratibu, kusimamia, kuendesha na kutathmini Mitihani ya Darasa la Nne na Saba, Kidato cha Nne na Sita, Mafunzo ya Ualimu pamoja na Mitihani ya Ufundikatika Mkoa kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Tanzania, OR-TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za Wathibiti Ubora wa Shule Kusimamia utekelezaji wa kazi za Maafisa Elimu wa Halmashauri waliopo katika Mkoa Kuratibu na kuchambua takwimu za Elimu katika Mkoa kwa ajili ya Mipango ya maendeleo katika ngazi za Halmashauri na Taifa Kusimamia na kuendesha uchaguzi wa Wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Kwanza katika Mkoa Kuratibu na kusimamia uhamisho wa wanafunzi wa Elimu ya Msingi na Sekondari ndani na nje ya Mkoa Kuratibu, kusimamia na kuendesha mashindano ya Taaluma katika ngazi ya Mkoa Kusimamia Mikutano ya Bodi inayohusu uendeshaji mipango ya maendeleo, nidhamu, mapato na matumizi ya fedha za shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu katika Mkoa kulingana na Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 kama ilivyorekebishwa mwaka 1995 kifungu cha 10 |
2. |
Florence Ngua
|
Afisa Elimu Taaluma Mkoa
|
Anawajibika kwa Mkuu wa Sehemu ya Elimu
Kufuatilia na kusimamia utekelezajiwa taarifa za Ukaguzi Kubuni Mipango ya kuinua kiwango cha taaluma katika Mkoa na kusimamia utekelezaji wake Kubuni mipango ya kuimarisha na kuendeleza taaluma ya Walimu na Wanafunzi, Kuratibu mashindano ya taaluma yanayoendeshwa katika Mkoa na Halmashauri Kuratibu utoaji wa huduma muhimu kwa wanafunzi kama vile mahudhurio, uhamisho na huduma za chakula, Kuratibu, kusimamia, kuendesha na kutathmini Mitihani ya darasa la Nne na Saba, Mafunzo ya Ualimu pamoja na Mitihani ya Ualimu na Ufundi katika Mkoa kwa kushirikiana na kamati za Mitihani ya Mkoa, Kushughulikia uhamisho wa wanafunzi wa Elimu ndani na nje ya Mkoa. Kubaini na kuratibu mafunzo endelevu ya walimu kazini na watumishi wengine wa shule za Msingi na Sekondari Kuhakikisha walimu wote wanafanyiwa tathmini ya wazi ya Utendaji kazi (OPRAS) KUratibu mashindano ya Michezo na Taaluma ya Shule za Msingi na Sekondari Kuhakikisha walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wanapangwa katika shule kwa kuzingatia Ikama inayokubalika |
3. |
Wilson Berthord
|
Afisa Elimu Taaluma
|
Anawajibika kwa Mkuu wa Sehemu ya Elimu
Kufuatilia na kusimamia utekelezajiwa taarifa za Ukaguzi Kubuni Mipango ya kuinua kiwango cha taaluma katika Mkoa na kusimamia utekelezaji wake Kubuni mipango ya kuimarisha na kuendeleza taaluma ya Walimu na Wanafunzi, Kuratibu mashindano ya taaluma yanayoendeshwa katika Mkoa na Halmashauri Kuratibu utoaji wa huduma muhimu kwa wanafunzi kama vile mahudhurio, uhamisho na huduma za chakula, Kuratibu, kusimamia, kuendesha na kutathmini Mitihani ya darasa la Nne na Saba, Mafunzo ya Ualimu pamoja na Mitihani ya Ualimu na Ufundi katika Mkoa kwa kushirikiana na kamati za Mitihani ya Mkoa, Kushughulikia uhamisho wa wanafunzi wa Elimu ndani na nje ya Mkoa. Kubaini na kuratibu mafunzo endelevu ya walimu kazini na watumishi wengine wa shule za Msingi na Sekondari Kuhakikisha walimu wote wanafanyiwa tathmini ya wazi ya Utendaji kazi (OPRAS) KUratibu mashindano ya Michezo na Taaluma ya Shule za Msingi na Sekondari Kuhakikisha walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wanapangwa katika shule kwa kuzingatia Ikama inayokubalika |
4. |
Beatrice Gati
|
Kaimu Afisa Elimu Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi
|
Anawajibika kwa Mkuu wa Sehemu ya Elimu
Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Watu wazima, Nje ya Mfumo Rasmi Kuratibu mahitaji na ugawaji wa rasilimali zihusuzo Elimu ya watu Wazima, Nje ya Mfumo Rasmi Kuratibu mashindano ya kitaaluma yanayoendeshwa katika Mkoa na Halmashauri kwa Elimu ya Watu Wazima, Nje ya Mfumo Rasmi Kuratibu utoaji wa Elimu Masafa na Ana kwa Ana kwa kushirikiana na Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoa na Waratibu wa Vituo katika Sekondari na Vyuo Kuratibu utoaji wa Elimu ya Sekondari katika Vituo vya Ufundi Stadi na vya Watu binafsi Nje ya Mfumo Rasmi Kuratibu mipango ya kufuta ujinga wa kutojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu inayoendeshwa na shule za Msingi na Sekondari Kutoa ushauri wa kiufundi kwa Serikali za Mitaa na Mashirika/Wadau katika kukuza na kuongeza uwezo wa kitaaluma katika kuboresha Elimu ya Watu Wazima, Nje ya Mfumo Rasmi na Elimu Maalum Kuratibu Mipango na kutayarisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Elimu ya watu Wazima, Nje ya Mfumo Rasmi na Elimu Maalum. |
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved