Bi. CHRISANTA SHAYO
Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu
MAJUKUMU YA KITENGO CHA FEDHA NA UHASIBU NA JINSIKINAVYOTEKELEZA MAJUKUMU YAKE
Kitengo cha Fedha na Uhasibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi kinatekeleza Majukumu Makuu matano. Majukumu hayo matano yameainishwa na kufafanuliwa jinsi yanavyotekelezwa na Wataalam waliopo kwenye Kitengo chaUhasibu na Fedha kama ifuatavyo:
Usimamiziwa Fedha:
Katika Usimamizi wa Fedha kitengo cha Fedha na Uhasibukinawajibika kuandaa na kuidhinisha malipo mbalimbali ya shughuli za kila sikuza uendeshaji wa ofisi pamoja na shughuli za kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoawa Katavi. Aidha, kitengo hiki kinawajibika katika kuandaa na kuidhinishamalipo ya Mishahara ya Watumishi, kuwezesha makato mbalimbali yanayokubalikakisheria kutoka kwenye mishahara ya watumishi na kuyawasilisha kwenye mamlakazinazohusika na makato hayo. Pia kutunza orodha na nyaraka za Watumishiwanaolipwa mishahara kwa ajili ya kumbukumbu za baadae.
KuwezeshaMalipo:
Katika Kitengo cha Fedha na Uhasibu tunawezesha malipombalimbali ya fedha kwa njia za kisasa ambazo ni za mtandao (yaani malipoyanafanyika kwa njia ya intaneti) ili kuondoa urasmu wa kuchelewesha malipo nakupelekea kukwamisha shughuli mbalimbali za Serikali, au kukwamisha malipombalimbali ya watumishi na malipo ya watoa huduma wanaotoa hudumambalimbali katika Serikali. Pia Kitengo kinawajibika kutunza daftari la hesabukwa ajili ya kumbukumbu za kimahesabu, Kupeleka benki fedha taslimu na hundibenki.
Hesabuza Mwisho wa Mwaka:
Kitengo cha Fedha na Uhasibu kinawajibika kutayarisha Makadirioya Bajeti na kudhibiti matumizi ya fedha pia kuandaa taarifa ya matumiziya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima kwa ajili ya kuiwasilisha kwa MhasibuMkuu wa Serikali. Kuandaa taarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka na kuziwasilishakwa Mhasibu Mkuu wa Serikali na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.Aidha, Kujibu hoja zote za ukaguzi na maoni ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali (CAG) pale anapokuwa amefanya ukaguzi wa fedha katika Ofisiya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
UkusanyajiMapato:
Kitengo cha Fedha na Uhasibu pia kinawajibika katika ukusanyajina usimamizi wa mapato ya Serikali kwa mujibu wa sheria na miongozo kwa baadhiya mali za Serikali zinazosimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na malihizo ni nyumba zinazomilikiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Ukaguziwa Awali:
Kitengo cha Fedha na Uhasibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavikinatekekeleza majukumu yake kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni namiongozo ya fedha ambapo kabla ya malipo hufanyika uhakiki wa nyaraka za malipokuona kama nyaraka hizo zimezingatia taratibu za malipo ikiwa ni pamoja nakuidhinishwa. Aidha, kuhakikisha malipo yanayofanyika hayavuki bajeti ya kasmahusika.
“Katavi: BilaUmaskini Inawezekana”
HAPA KAZI TU
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved