UTANGULIZI
TEHAMA ni moja ya kitengo kinachounda Sekretariati ya Mkoa wa Katavi. Jukumu kubwa la kitengo hiki ni kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa kuhusu shughuli zote za Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano katika Mkoa wa Katavi.
MAJUKUMU YA KITENGO:
Lengo
Kutoa ushauri na utaalam kuhusu masuala yahusuyo TEHAMA .
Kitengo kitafanya kazi zifuatazo:-
Utekelezaji wa sera ya TEHAMA na Serikali mtandao;
Kushauri matumizi sahihi ya miongozo mbalimbali ya TEHAMA iliyotolewa na Serikali katika kusimamia mifumo ya kielektironiki kwa ufanisi na weledi.
Kushauri kuhusu manunuzi ya vifaa vya TEHAMA vinavyozingatia ubora na viwango vinavyokubalika.
Kutoa huduma za ushauri wa kitaalam na msaada wa kiufundi kwa ngazi ya Mkoa na Halmashauri zake zote kadri inavyohitajika.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved