Kitengo hiki kina lengo la kuleta ufanisi na kutoa huduma kwenye nyanja za manunuzi, utunzaji na usambazaji wa bidhaa na huduma mbalimbali zinazohitajika kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa. Kitengo hiki kinaongozwa na Afisa Ugavi Mkuu ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
Kushauri uongozi juu ya masuala yanayohusiana na manunuzi ya bidhaa na huduma na mchakato mzima wa kusimamia na kudhibiti mwenendo wa bidhaa na huduma katika Mkoa.
Kuhakikisha kwamba Mkoa unafuata/unatii taratibu za manunuzi kulingana na sheria ya Manunuzi ya Umma
Kuandaa na kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Mwaka wa Manunuzi kwa ajili ya Mkoa
Kununua, kuhifadhi na kusimamia usambazaji, vifaa na huduma mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya bidhaa na huduma hizo kwenye Mkoa
Kuhakikisha kunakuwepo na utunzaji, uhifadhi sahihi na usambazaji wa mahitaji ya ofisi wa kutosheleza na kwa wakati
Kutunza na Kuboresha kumbukumbu ya vifaa na rasilimali za serikali/za ofisi
Kushughulikia uratibu wa kikao cha bodi ya manunuzi ya Mkoa kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013