Mkoa umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) kwa kujenga jumla ya zahanati 21 na hivyo kuongeza idadi ya zahanati kutoka 59 mwaka 2012 hadi kufikia zahanati 69 mwaka 2016. Mkoa umefanikiwa pia kuongeza idadi ya vituo vya afya kutoka 11 mwaka 2010 hadi kufikia vituo 13 mwaka 2017. Mkoa bado una Hospitali moja ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda. Hata hivyo ujenzi wa Hospitali ya Mkoa umeanza na utaratibu wa kutoa ithibati ya kituo cha Afya Inyonga kuwa Hospitali ya Wilaya umefikia hatua za mwishoni baada ya Halmashauri kukamilisha maelekezo yaliyotolewa na Wizara.
Halisi ya vituo vya kutolea huduma za afya
Halmashauri | Zahanati | Vituo vya Afya | Hospitali | Jumla | ||||||||
Ser | Bin | JML | Ser | Bin | JML | Ser | Bin | JML | Ser | Bin | JML | |
Manispaa ya Mpanda | 6 | 9 | 15 | 2 | 1 | 3 | 1 | 0 | 1 | 9 | 10 | 19 |
H/W Mpanda | 17 | 1 | 18 | 3 | 0 | 3 | 0 | 0 | 0 | 20 | 1 | 21 |
H/W Mlele | 6 | 1 | 7 | 1 | 0 | 1 | 0 | 0 | 0 | 7 | 1 | 8 |
H/W Nsimbo | 17 | 0 | 17 | 3 | 1 | 4 | 0 | 0 | 0 | 20 | 1 | 21 |
H/W Mpimbwe | 10 | 2 | 12 | 2 | 0 | 2 | 0 | 0 | 0 | 12 | 2 | 14 |
Jumla | 56 | 13 | 69 | 11 | 2 | 13 | 1 | 0 | 1 | 68 | 15 | 83 |
Mkoa umeendelea kuboresha huduma za mama na mtoto na kuhakikisha kuwa afya ya mama inaimarika wakati wa ujauzito. Kutokana na uboreshaji huu idadi ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya imeongezeka kutoka akinamama 17,334 mwaka 2012 sawa na asilimia 50 hadi kufikia akinamama 21,176 mwaka 2016 sawa na asilimia 79. Vifo vya watoto waliochini ya miaka mitano vimepungua kutoka watoto 83 kati ya vizazi hai 1000 mwaka 2012 hadi kufikia 24 kati ya vizazi hai 1000 mwaka 2016, wastani wa kitaifa ni 54 kati ya vizazi hai 1000. Idadi ya vifo vya akinamama wajawazito vimepungua kutoka vifo 292/100,000 mwaka 2012 hadi kufikia vifo 189/100,000 mwaka 2016.
Mkoa umefanikiwa kupunguza kasi ya ugonjwa wa malaria kwa asilimia 6 mwaka 2015 kutoka asilimia 10 mwaka 2012, Lengo ikiwa ni kufikia asilimia 1 ifikapo mwaka 2020. Aidha, jumla ya kaya 102,320 ziligawiwa vyandarua vyenye viuatilifu vya kudumu muda mrefu (LLINS) mwaka 2012 ikilinganishwa na kaya 164,756 zilizopewa vyandarua vyenye viuatilifu vya kudumu muda mrefu (LLINs) mwaka 2015 kati ya kaya zilizokadiriwa 159,390 hivyo mkoa umefanikiwa kuvuka lengo kwa asilimia 103
Huduma huduma za chanjo zinazotolewa.
AINA YA CHANJO | WALENGWA | WALIOCHANJWA | ASILIMIA | MAELEZO |
BCG | 30,100 | 53780 | 179 | Lengo la kitaifa lilifikiwa |
PENTA 3 | 27538 | 33170 | 120 | Lengo la kitaifa lilifikiwa |
POLIO | 27538 | 31072 | 113 | Lengo la kitaifa lilifikiwa |
SURUA | 27538 | 16212 | 59 | Lengo la kitaifa halikufikiwa kutokana na upungufu wa chanjo nchini kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili |
Mkoa umeendelea kuratibu mpango wa matunzo na matibabu kwa watu wanoishi na virusi vya UKIMWI ambapo jumla ya watu 5,240 waliweza kugundulika na maambukizi na wakaandikishwa katika vituo vya Tiba na Matunzo. Wagonjwa 10,380 (watu wazima 9754 na watoto 616) wapo katika dawa. Aidha, katika huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto wakati wa ujauzito, kujifungua na kunyonyesha. Mwaka 2012 Mkoa ulikuwa na jumla ya vituo 49 kati ya 72 vina wataalam waliofundishwa na vinatoa huduma na kufikia vituo 70 kati ya 83 vya kutoa huduma za Afya katika Mkoa kwa mwaka 2016. Aidha, hali ya maambukizi ya UKIMWI yamepungua kutoka asilimia 5.9% mwaka 2012 mpaka asilimia 4.1% mwaka 2016.
Huduma za Wazee
Mkoa kupitia Halmashauri zake umekuwa ukitoa huduma ya matibabu bila malipo kwa wazee. Mkoa umefanikiwa kutoa jumla ya vitambulisho vya kudumu 1807 kati ya wazee 19,248 waliotambuliwa. Licha ya vitambulisho hivyo Halmashauri zinatoa huduma za wazee kwa kuwapatia barua za utambulisho kutoka katika Serikali za vijiji na mitaa wanakoishi.
Huduma za Afya kupitia CHF
Hadi kufikia mwezi Desemba 2016 Mkoa una jumla ya wanachama 42,259 ambao ni sawa na asilimia 39.6 ambao wamejiunga na CHF. Mkoa umeendelea kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za afya kupitia vituo vinavyotoa huduma za afya katika maeneo yao. Kutokana na hamasa hiyo idadi ya wanufaika wa Mfuko wa Afya wa jamii (CHF) imeongezeka kutoka asilimia sita (6) mwaka 2012 hadi asilimia 39.6 Desemba 2016. Katika jitihada za kuimarisha ukusanyaji wa mapato yatokanayo na uchangiaji wa huduma za afya, Mkoa umeendelea kuzielekeza Halmashauri kufunga na kutumia mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji wa mapato. Katika kuteleza agizo hilo, Hospitali ya Manispaa ya Mpanda imeanza kutumia mfumo wa kieletroniki.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved