MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU WATANZANIA WAPYA WALIOPEWA URAIA KATIKA MAKAZI YA KATUMBA, MISHAMO NA ULYANKULU.
Serikali imeweka wazi msimamo wake kuwa inaweza kuwafutia uraia watanzania wapya waliopewa uraia wale ambao walikuwa wakimbizi wanaoishi makazi ya katumba Mishamo na Ulyankulu iwapo wataonekana kushindwa kufuata sheria za nchi na kujihusisha na vitendo vya uharifu na uvunjifu wa sheria za nchi na kusisitiza vitendo vya ubaguzi wenyewe kwa wenyewe ubaguzi wa kitabaka kubaguana kisiasa,kidini na kwa namna yeyote hawawezi kuvumiliwa hata kidogo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameki Nchemba wakati akiwahutubia raia hao wapya kwenye Makazi ya Katumba iliyoko katika Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi ikiwa ni pamoja na kusisitiza kujiepusha na vitendo vya kubaguana.
Akizungumzia kuhusu Uzalendo wa kuipenda nchi asisitiza na kuwataka raia hao kuepukana na tabia ya za chuki dhhidi ya nchi yako badala yake uzalendo uwe mbele kwanza kwa nchi.
Mapema Mhe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amesema kuhusu suala la maeneo ya makazi kufutwa hati ya kuwa makazi, amesema eneo hilo haliwezi kufutwa hati ya kuitwa makazi hadi taratibu za kuhakikisha wale wote wanaoishi katika makazi hayo ni raia wa Tanzania na hakuna mkimbizi katika maeneo hayo lakini kama kutakuwa bado wapo wakimbizi hati haiwezi kubadilishwa hadi taratibu zikamilike.
Pia amewasisitisitiza kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yao.
Mapema Mkuu wa Makazi ya Mishamo na Katumba Athman Igwe alieleza kuwa kata ya Katumba ni ya muda mrefu na ilianzishwa mwaka 1972 hadi kufika sasa kuna wakazi zaidi ya 78,000 lakini asilimia tisini na saba ni ya raia wapya hivyo bado kuna wakimbizi kwenye eneo hili.
Hivi karibuni kulikuwa na zoezi la kuhakiki wakimbizi kwa ajili ya kuwatafutia ufumbuzi wa kudumu zoezi lilianza tarehe 16 mwezi wa saba na limekamilika kwenye makazi haya mapya mwaka huu tarehe 3/8/ 2017 waliosajiliwa waliohakikiwa ni wakimbizi 11,329 kwa maana hiyo kuna kaya 5,134.
Pia Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewaasa watanzani wapya wanaoishi makazi ya Katumba na Mishamo Mkoani Katavi kuondoa fikra ya kuwa wao bado ni wakimbizi badala yake wawe huru kwenda kuishi sehemu yeyote katika nchi maadamu wafuate taratibu na kuwasisitiza wale ambao hawajachukua vyeti vyao vya uraia wavichukue .
Akihutubia kwenye mkutano wa Hadhara katika makazi ya Katumba na Mishamo Waziri Mwigulu ameeleza,na kuwasisitiza raia hao wapya na wale waliopatiwa vyeti vya uraia lakini hawataki kuchukua vyeti vyao waamue moja ama wachukue au waondoke kurudi kwao kwa kuwa kulikuwa hakuna haja ya kuomba uraia huo kama walikuwa hawautaki.
Akizungumzia kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine katika nchi hii amesema ni jambo jema lakini amewaomba wasibadili majina yao bila kufuata utaratibu
Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amewaasa kutunza mazingira pamoja na kusisitiza suala la kujitokeza kujiandisha kwa wale ambao hawakuandikishwa.
Mapema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Saidi Mselem amemweleza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa wananchi wa Mishamo na Katumba wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika maeneo hayo kwa kuwa wako watanzania wapya na wale walioandikishwa.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved