1.1 Historia ya Mkoa
Mkoa wa Katavi una ukubwa wa kilomita za mraba 47,527 na ulitangazwa rasmi tarehe 01 Marchi, 2012 kwa uamuzi wa serikali wa kuanzisha Mikoa minne mipya ambayo ni (Katavi, Njombe, Simiyu na Geita) kwa lengo la kusogeza huduma za ki-utawala na Ki-uchumi kwa wananchi wake na ulizinduliwa rasmi tarehe 25/11/2012 na Mheshimiwa Gharib Bilal, Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Amri ya Serikali ya maeneo ya kiutawala ya mwaka 2019, Mkoa wa Katavi una maeneo ya Kiutawala yafuatayo:-
S/N |
WILAYA |
HALMASHAURI |
TARAFA |
KATA |
VIJIJI |
VITONGOJI |
MITAA |
JIMBO |
01 |
Mpanda
|
MPANDA MC
|
2 -Kashaulili na Misunkumilo. |
15 |
14 |
81 |
43 |
MPANDA MJINI
|
|
|
NSIMBO DC
|
2-Nsimbo na Ndurumo |
12 |
59 |
272 |
- |
NSIMBO
|
02 |
Tanganyika
|
MPANDA DC
|
3-Karema, Kabungu na Mwese. |
16 |
55 |
328 |
- |
MPANDA VIJIJINI
|
04 |
Mlele
|
MLELE DC
|
1-Inyonga |
6 |
18 |
85 |
- |
KATAVI
|
05 |
|
MPIMBWE DC
|
2-Mpimbwe na Mamba |
9 |
31 |
165 |
- |
KAVUU
|
|
JUMLA
|
|
10 |
58 |
177 |
931 |
43 |
5 |
1.2 Mipaka ya Mkoa na Mahali Ulipo
Mkoa upo Magharibi mwa Tanzania kati ya Latitude 40 na 80 kusini mwa msitari wa Ikweta na Longitude 300 hadi 330 Mashariki mwa msitari wa Greenwich. Mipaka yake ni kama ifuatavyo:
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Mkoa una jumla ya wakazi 564,604, kati ya hao wanawake 289,817 na wanaume 274,787. Wastani kwa kaya moja ni watu 6 na uwiano wa kijinsia ni asilimia 98. Aidha, ongezeko la idadi ya watu ni asilimia 3.2 kwa mwaka. Mwaka 2016 Mkoa unakadiriwa kuwa na jumla ya watu 649,837 wanawake 327,934 na wanaume 321,903. Katika idadi hiyo kundi la nguvukazi ambao ni watu wenye umri wa miaka kati ya 15 na 64 wako 297,248.
Mkoa upo kati ya wastani wa mita 1000 hadi 2500 kutoka usawa wa bahari. Hali ya joto I kati ya nyuzi 130c ma 160c miezi ya Juni na Julai na nyuzi 260c hadi 300c miezi ya Septemba hadi Novemba. Kwa wastani, hupata mvua kati ya mm 700 hadi mm 1300 zinazonyesha kati ya Novemba na April. Mkoa umegawanyika katika kanda 4 za hali ya hewa ambazo ni ukanda wa bonde la ziwa Rukwa, Nyanda za uoto wa miombo ya Katumba-Inyonga, Miinuko ya Mwese na Mwambao wa ziwa Tanganyika.
Jedwali 1: Kuonesha Kanda, Eneo, Mwinuko, Kiwango cha Mvua na Shughuli za Kiuchumi.
Kanda
|
Eneo
|
Mwinuko
|
Udongo na kiwango cha mvua
|
Shughuli za Kiuchumi
|
Uwanda wa Katumba
|
Tarafa ya Nsimbo
|
1000-1500m
|
Udongo-udongo tifutifu unaopitisha maji kirahisi Mvua – 92mm-1000mm
|
1. Kilimo
Mahindi, Mihogo, Tumbaku , Maharage, Karanga, Alizeti & Miwa 2. Mifugo Ng’ombe, Kondoo, Mbuzi, Kuku. |
Nyanda za Mwese
|
Tarafa ya Mwese
|
1100-2500m
|
Udongo- udongo kichanga (Hilly)
Mvua- 100 -1100 |
1. Kilimo
Mahindi, Mihogo, Maharage, Ndizi, Kahawa, Viazi mviringo 2. Mifugo Ng’ombe, Kondoo,Mbuzi,Kuku (poultry) 3. Nyinginezo: ufugaji nyuki |
Bonde la Karema
|
Tarafa ya Karema
|
1000-1300m
|
Udongo – Udongo wa kichanga
Mvua kiasi cha 1200mm. |
1. Kilimo
Mahindi, Mhogo na Mpunga 2. Mifugo Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku 3. Mengineyo Uvuvi & Mbao |
Bonde la ziwa Rukwa
|
Mpimbwe
|
Mwinuko unaanzia 1000-1100m upande wa kaskazini na 800 – 900 ufukweni wa Ziwa Rukwa.
|
Udongo- Udongo wa kichanga unaopitisha maji kidogo
Mvua – inanyesha kuelekea kusini kwa kiasi cha 1250 mm kwa mwaka hadi 840 mm-970mm chini ya miinuko ya Lyambalyamfipa . |
1. Kilimo,
Mahindi, Mpunga, Matunda, (Horticulture), Mhogo, Ulezi, Mtama. 2. Mifugo Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo & Kuku Nyingineyo Uvuvi & Mbao |
Ziwa Tanganyika
|
Karema
|
770-1300
|
Udongo – Kichanga unaopitisha maji.
Mvua 950-1200mm |
1.Kilimo
Mahindi, Mhogo, Michikichi, Mpunga 2. Mifugo Ng’ombe, Mbuzi na kondoo 3. shughuli Nyingineyo Uvuvi |
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved