Katika Mkoa wa Katavi sekta ya mifugo ina nafasi kubwa katika kuchangia upatikanaji wa lishe bora, ajira, kipato kwa wananchi na pato la Taifa kwa ujumla kwa njia ya biashara ya mifugo hai na mazao yake. Pia sekta ya mifugo huchangia kwa kiwango kikubwa katika kuongeza uzalishaji wa mazao kupitia matumizi ya wanyama kazi na samadi ambayo hutumika kurutubisha ardhi.
Uchumi wa Mkoa unategemea zaidi kilimo (ufugaji na uzalishaji mazao) ambacho kinachangia asilimia 90 ya pato la Mkoa pia kinaajiri zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wote. Mifugo inayofugwa ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku, bata, kanga, njiwa, sungura, nguruwe, paka,mbwa na punda.
Kwa sasa Mkoa una jumla ya ng’ombe 501,203, mbuzi 147,173, kondoo 45,414 nguruwe 14,813, kuku 630,057, bata 39,657, punda 918, njiwa 24,426, Kanga 1,863, Sungura 954 na ndezi panya 736 (Jedwali Na. 1).
Fursa za uwekezaji katika Sekta ya Mifugo
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved