Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akishiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi nyumbani kwake mara baada ya Karani wa Sensa kufika kwa ajili ya zoezi hilo 23 Agosti 2022.
Mpanda-Katavi
Zoezi la Sensa ya watu na makazi lililoanza rasmi Tarehe 23 Agusti 2022 limeendelea kupokelewa kwa muitikio mkubwa na Wananchi Mkoani Katavi huku viongozi mbalimbali wa Kimkoa na Wilaya wakiwaongoza Wananchi kushiriki Sensa katika maeneo yao.
Zoezi la Sensa ya watu na makazi Mkoani Katavi lilianza kutekelezwa saa Sita usiku ambapo makarani wa Sensa walipita katika maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko kama vile Vituo vya Mabasi,Kumbi za Starehe,Nyumba za Kulala wageni,Magereza,Polisi pamoja na baadhi ya Kaya ambapo katika maeneo hayo kumekuwa na muitikio mkubwa na utayari wa Wananchi kuhesabiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko aliwaongoza Wananchi Mkoani humo kuhesabiwa ambapo karani wa Sensa alifika nyumbani kwake majira ya Saa 3:00 asubuhi na kuanza kutekeleza zoezi hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kushiriki Sensa Mhe.Mrindoko amesema zoezi hilo limefanyika kwa utulivu mkubwa pasi kuwepo na changamoto yoyote.
Amewashukuru wadau mbalimbali walioshiriki kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi Mkoani Katavi ambapo
Mhe.Mrindoko amewataka Wananchi Mkoani humo kutoa ushirikiano kwa viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuacha Taarifa sahihi kwa watakaobaki katika kaya ili kurahisisha shughuli za ujazaji wa madodoso kwa makarani wa sensa katika Kaya zao.
Aidha amesisitiza utoaji wa taarifa sahihi kwa makarani wa Sensa ili kuiwezesha Serikali kuwa na taarifa sahihi zitakazowezesha kupanga Mipango mbalimbali ya maendeleo
Mhe.Mrindoko pia ametembelea baadhi ya Kaya katika manispaa ya Mpanda kwa lengo la kujiridhisha namna ambavyo zoezi hilo la Sensa linatekelezwa katika maeneo mbalimbali ambapo pia amekutana na kuzungumza na Wafanyabiashara katika soko kuula Mpanda ambapo alitoa elimu kuhusu Sensa kwa Wananchi hao.
Kwa Upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa baada ya kushiriki kuhesabiwa amesema zoezi hilo litafanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuwa maandalizi yalifanyika kwa asilimia 100.
Nao Wananchi mbalimbali walioshiriki kuhesabiwa wameipongeza Serikali kwa maboresho ya zoezi la Sensa amnbapo kwa sasa wameshuhudia zoezi hilo likidodosa taarifa nyingi zaidi kwa kutumia TEHAMA.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved