Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akikabidhi hundi ya zaidi ya Shilingi Milioni Mia tatu kwa vikundi 14 vya Wajasiriamali wa makundi ya Wanawake,Vijana na wenye Ulemavu zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa wajasiriamali ikiwa ni utekelezaji wa utengaji wa fedha Asilimia 10 za mapato ya ndani Agosti 11,2022.
Shilingi Milioni mia tatu arobaini na mbili Laki tatu na hamsini na tisa zimetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa vikundi 14 vya wajasiriamali wa makundi ya Wanawake,Vijana na wenye ulemavu, iikiwa ni utekelezaji wa utengaji wa fedha asilimia 10 kwa ajili ya Wanawake,Vijana na wenye ulemavu katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022.
Akikabidhi hundi ya fedha hizo, kwa wajasiriamali hao mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko, amewataka wanufaika wa mikopo iliyotolewa kuzingatia vigezo na masharti yaliyotolewa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafanya marejesho kwa wakati ili kuepuka usumbufu.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bi Halima Kitumba ameeleza kuwa kiwango hicho cha fedha kilichotolewa kimetokana na fedha za marejesho pamoja na makusanyo ya ndani ya Halmashauri.
Ameeleza kuwa uwepo wa mikopo hiyo kwa makundi maalumu imesadia kwa kiwango kikubwa kuwaondoa vijana wengi kutoka katika makundi hatari ya matumizi ya madawa ya kulevya na vitendo vingine vya utovu wa kimaadili vinavyosababishwa kwa sehemu kubwa na ukosefu wa Ajira.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved