Pichani:Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe.Filberto Sanga alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko katika uzinduzi wa Wiki ya Mwakakatavi katika uwanja wa Shule ya Msingi Kashato 28 Oktoba 2022
Mpanda.
Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kutumia fursa ya maonyesho ya Wiki ya Mwanakatavi kujifunza masuala mbalimbali ya Kilimo na Utalii ili kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika Skta ya kilimo na utalii kujikwamua Kiuchumi.
Rai hiyo imtolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw.Filberto Sanga kwa niaba ya Mkuu wa wa Katavi Bi.Mwanamvua Hoza Mrindoko katika uzinduzi wa maonyesho ya Kilimo na Utalii ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Mwanakati ya Kilimo na Utalii iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashato Manispaa ya Mpanda
Bw.Sanga amewahimiza Wananchi kutumia vyema manyesho hayo kujifunza fursa mbalimbali katika Sekta ya Kilimo na Utalii zinazopatikana ndani ya Mkoa wa Katavi jambo litakalosaidia kuimarisha uchumi wa Mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Aidha Bw.Sanga ametoa rai kwa Taasisi za Uhifadhi wa Maliasili Mkoani Katavi kuelekeza nguvu ya ziada katika ulinzi wa Maliasili hizo ikiwemo Misitu na Wanyamapori ili kunusuru rasilimali hizo dhidi ya Wavamizi.
Amewataka Maafisa Ugani Mkoani Katavi kuhakikisha wanawasajili wakulima wote kwa kuwa lengo la zoezi hilo licha ya kufanikisha zoezi la uuzaji wa mbolea ya ruzuku pia linalenga kutambua idadi ya Wakulima wote Nchini.
Katika hatua nyingine Bw.Sanga amelitaka shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo Nchini SIDO kujenga uwezo kwa Wajasiriamali juu ya namna ya kukuza mitaji yao ili kujikwamua na Umasikini.
Awali Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Nehemia James katika ufunguzi wa Maonyesho ya Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii amesema lengo la maonyesho hayo ni kutoa fursa kwa Wananchi Mkoani humo kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Kilimo na Utalii pamoja na kubaini fursa zilizopo katika Sekta hizo.
Amesema maonyesho hayo yatadumu kwa muda wa siku 5 baada ya uzinduzi ambapo Washiriki 28 zikiwemo Taasisi mbalimbali za Kiserikali,Mashirika binafsi pamoja na Wajasiriamali wadogo Wanashiriki katika maonyesho hayo.
Aidha katika kuadhimisha Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii baada ya uzinduzi Wananchi watapata fursa ya Kushuhudia Shindano la Kusaka Miss Utalii Katavi jioni katika ukumbi wa Mpanda Social ambapo siku ya 30 Oktoba 2022 kutakuwa na tukio la kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii ndani ya Mkoa wa Katavi ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na Shamba la Mbuni,ikitafuatiwa na tukio la Uzinduzi wa Filamu ya The Royal Tour Mkoani Katavi jioni katika ukumbi wa Mpanda Social.
Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Mlele akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi ametembelea na kukagua mabanda ya maonyesho ya Taasisi mbalimbali na mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na Wajasiriamali wadogo ambapo maadhimisho hayo yanatarajiwa kufungwa rasmi siku ya Tarehe 2 Oktoba 2022.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved