Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko alipotoa Taarifa ya ujio wa Ugeni wa Mhe.Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kwa Waandishi wa Habari(Hawako pichani) Wilayani Mlele katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo 10 Disemba 2022.
Na:OMM -Mkoa
Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa Majaliwa atafanya Ziara ya siku 3 Mkoani Katavi, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko ameeleza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Wilayani Mlele Mhe.Mrindoko ameeleza kuwa Mhe.Waziri Mkuu Kasim Majaliwa atawasili Mkoani Katavi siku ya Jumatatu Tarehe 12 Desemba 2022 ambapo atapokelewa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda.
Akiwa Mkoani Katavi Mhe.Waziri Mkuu atakagua,kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi Miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo pia atasalimiana na Wananchi,pamoja na kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Katavi.
Siku ya Tarehe 12 Disemba, 2022 baada ya kuwasili Mhe.Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Majaliwa (Mb) ataelekea Wilayani Tanganyika kwa ajili ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Akiwa Wilayani Tanganyika Mhe.Waziri Mkuu atazindua mradi wa Maji katika Kijiji cha Vikonge kilichopo Kata ya Tongwe na baada ya hapo ataelekea katika Kata ya Sibwesa kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Sibwesa.
Baada ya hapo Mhe.Waziri Mkuu ataelekea Kata ya Kasekese kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi katika Zahanati ya Kagunga na Madarasa Mawili.
Siku ya Tarehe 13 Disemba, 2022 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa Majaliwa (Mb) ataweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na kisha kuelekea Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika eneo la Kabatini kwa ajili ya kutembelea Shamba la Korosho na Mahindi.
Baada ya hapo Mhe.Waziri Mkuu ataelekea Nsimbo Senta ambapo atakagua na kuzindua Kiwanda cha Maziwa cha MMS.
Baada ya hapo Mhe.Waziri Mkuu ataelekea Rungwa Manispaa ya Mpanda kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, na kisha atazungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Katavi katika Ukumbi wa Mpanda Social.
Aidha Siku ya Tarehe 14 Disemba 2022 Mhe Mrindoko ameeleza kuwa Mhe.Waziri Mkuu ataelekea Wilayani Mlele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe kutembelea Kituo cha Afya Majimoto kilichijengwa kwa fedha za tozo pamoja na kuzindua matumizi ya Kituo hicho.
Akiwa Mpimbwe Mhe.Waziri Mkuu atahitimisha ziara yake kwa kufungua na kukagua Ujenzi wa Madarasa 13 ya Shule ya Sekondari Majimoto pamoja na kusalimia Wananchi wa Majimoto.
Mhe Mrindoko ametoa wito kwa Wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya ugeni huo mkubwa wa Kitaifa wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amewataka Viongozi wa ngazi zote kujipanga vyema pamoja na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Mhe.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved