Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi Jamila Y.Kimaro Mkataba wa usimamizi na Utekelezaji wa Afua za Lishe mara baada ya kusaini mikataba hiyo 10 Oktoba 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko amewataka Wakuu wa Wilaya,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri kuchukua hatua Kali Kwa Maafisa watakaoshindwa kutekeleza shughuli za uboreshaji Afua za Lishe Mkoani humo.
Mhe. Mrindoko ametoa kauli hiyo katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mpango mkakati wa usafi na utunzaji mazingira mkoa wa Katavi,kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ulioko Mpanda Mjini.
"Hatutakubali kuendelea kufanyana nae kazi,itabidi apumzike pembeni tutafute Watumishi ambao watasimamia vizuri afua hii ya lishe"
Awali akitoa taarifa ya hali ya Lishe Mkoani humo Afisa Lishe mkoa wa Katavi Asnath Mrema amesema Mkoa wa Katavi uko nafasi ya 14 Kitaifa.
Amesema moja ya sababu ya Mkoa huo kushika nafasi ya 14 ni kutokana na Halmashauri za Mkoa huo kushindwa kutoa fedha za afua za Lishe kama ilivyoainishwa kwenye Bajeti na mipango.
Katika hatua za makusudi,RC Mrindoko amesainiana na kukabidhi mikataba ya Lishe na wakuu wa Wilaya za mkoa huo lengo likiwa ni utekelezaji wa kupambana na lishe duni kuanzia ngazi ya Wilaya hadi ngazi ya kitongoji.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved