Pichani:Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassa Abas Rugwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ys UKIMWI Duniani alipotoa hotuba yake katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kasekese wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMW Duniani 1 Desemba 2022.
Tanganyika,
Viongozi,Wataalamu pamoja na wadau mbalimbali Mkoani Katavi wametakiwa kuelekeza nguvu zaidi katika kutoa Elimu juu ya umuhimu wa kupima Virusi vya UKIMWI na kutambua hali ya Afya zao ili kuchukua hatua stahiki na kwa wakati ili kuepuka Afya kutetereka.
Rai hiyo imetolewa na Katibu tawala mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika Shule ya msingi Kasekese Kata ya Kasekese Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Katibu Tawala Rugwa ameeleza kuwa kutokana na hali ya maambukizi ya VVU kuwa Asilimia 5.9 katika Mkoa wa Katavi, ambayo ni kiwango cha juu ikilinganishwa na kiwango cha maambukizi ya VVU cha Taifa ambacho ni Asilimia 4.7 ni muhimu kama Mkoa kujipanga.
“Sisi kama Mkoa tuna kila sababu ya kuhakikisha kuwa tunafanya jitiada za makusudi kushusha kiwango cha maambukizi walau kifikie kiwango chini ya wastani ule wa Taifa kama ambavyo baadhi ya Mikoa ya wenzetu wamefanikiwa kushusha”Alisema Katibu Tawala Rugwa.
Awali akiwasilisha Taarifa mbele ya Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dokta Omari Sukari amesema Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali umefanikiwa kutekeleza Afua mbalimbali za kupambana na UKIMWI ambapo Mkoa umefanikiwa kufikia Malengo ya Tisini na tano ya kwanza kwa Asilimia 111.1,kufikia malengo ya Tisini na tano ya Pili kwa Asilimia 96.9.
Aidha Dokta Sukari ameeleza kuwa Idadi ya Vituo vya kutolea huduma za tiba na malezi kwa watu wanaoishi na VVU (CTC) imeongezeka kutoka vituo 34 mwaka 2020 hadi vituo 51 kufikia Septemba, 2022.
Ameongeza kuwa Idadi ya Vituo vya kutolea huduma za ushauri nasihi na upimaji wa VVU imeongezeka kutoka vituo 76 mwaka 2020 hadi vituo 83 kufikia Septemba 2022.
Katika maadhimisho hayo ya siku ya UKIMWI Duniani iliyobeba kaulimbiu inayosema Imarisha Usawa yamefana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kasekese ambapo shughuli mbalimbali zikiwemo upimaji wa Afya pamoja na Elimu kuhusu masuala mbalimbali ya Afya zimefanyika kwa Mafanikio makubwa.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved