Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Florence Chrisant, amewataka viongozi wa dini kutumia madhabahu kutoa elimu na kukemea vitendo vya rushwa, hasa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025. Amesisitiza umuhimu wa kuhubiri amani na kutoa taarifa kwa vyombo husika pindi viashiria vya uvunjifu wa sheria vinapojitokeza.
Kauli hiyo ameitoa Julai 18, 2025, wakati wa warsha iliyoandaliwa na TAKUKURU kwa lengo la kuwajengea uelewa viongozi wa dini kuhusu nafasi yao katika mapambano dhidi ya rushwa wakati wa uchaguzi.
Akizungumza katika warsha hiyo, Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi, Bw. Stuart Kiondo, amesema viongozi wa dini wana ushawishi mkubwa kwa jamii na hivyo wanapaswa kutumia sauti zao kuhimiza maadili mema na kukemea rushwa majukwaani.
Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Katavi, Sheikh Mashaka Kakulukulu, amepongeza TAKUKURU kwa kushirikisha viongozi wa dini, akisisitiza kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni jukumu la kila mmoja, si serikali pekee.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved