Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Jamila Yusuph amemuakilisha Mhe. Mwanamvua Mrindoko Mkuu wa Mkoa wa Katavi Katika
Uzinduzi Rasmi wa zoezi la utoaji wa Mikopo ya Asilimia 10% kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu, ambazo ni Fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri na kutoa Hundi ya Mfano yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.3.
"Natoa pongezi kwa Vikundi vyote , Fedha hizo mkazitumie kulingana na Malengo mliyojiwekea. Mkoa wa Katavi unaenda kutoa Fedha Bilioni 2.3 kwa vikundi vitatu, Wanawake , Vijana na Watu wenye Ulemavu, mkazitumie vizuri Ili mkatimize Malengo yenu". Amesema Mhe. Jamila Yusuph.
Mhe. Jamila amewasihi wote walioomba na watakaopata Mikopo hiyo kuzingatia kanuni, taratibu na Sheria za Mikopo ili ikatoe matokeo chanya katika shughuli wanazoenda kuzifanya na kutimiza azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha vikundi mbalimbali vya wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu vinajikwamua kiuchumi.
Akizungumza mala baada ya Uzinduzi huo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda, Mhe. Haidari Sumry amesema kuwa vikundi vyote vilivyopewa mikopo vifanye kazi iliyokusudiwa ili viweze kunufaika na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati, ili kundi lingine liweze kunufaika na mikopo hii.
"Serikali imeamua kurejesha mikopo hii ya asilimia 10 ya Vijana, Wanawake na watu wenye Ulemavu, ikiwa na dhamira ya kutoa ajira na kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wa Mkoa wetu kwa ujumla". Amesema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kikundi cha Boda Boda Wilaya ya Mlele Bwana Joshua Gabriel Mosses amesema, "Tunapenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe .Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuyakumbuka makundi yote na kuyawewezesha kupata mikopo hii kwa awamu nyingine toka isitishwe.
"sisi kama wana kikundi tutautumia vizuri mkopo huu na kuhakikisha tunarejesha kwa wakati ili wanufaika wengine wapate fursa hii". Amesema.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumanne tarehe 10 Desemba katika Ukumbi wa Mpanda Social Hall uliopo Manispaa ya Mpanda.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved