RC Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko akipata upimaji na ushauri wa hali ya vision ya macho yake katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi. Kitendo hicho ni ishara ya uzinduzi wa huduma za afya za kibingwa zinazoendelea kutolewa na madaktari bingwa kutoka Hosptali ya Benjamin Mkapa. Katika uzinduzi huo, Mhe. Mrindoko amewahakikishia wananchi wote waliojitokeza kuwa wote watapata huduma, hakuna hata mtu mmoja atakayeachwa, wote watapata matibabu ya maradhi yanayowasumbua. Wananchi wote mnaalikwa kuchangamkia huduma hizo ambazo kuzipata mpaka ufike Benjamin Mkapa Hospital au Hospitali zingine zinazotowa huduma za afya za kingwa nchini.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved