Miti ya Mikorosho ina faida nyingi. Hutupatia chakula, kipato( binafsi na kwa serikali) na hutunza mazingira kama mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi Tanzania na ulimwengu wa ujumla. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inahamasisha wananchi kupanda mikorosho katika maeneo ambayo mikorosho inaweza kustawi. Kwa muktadha huo, Kiongozi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko anajitokeza kugawa miche ya mikorosho bure kwa wananchi wake kwa ajiili ya kupanda katika mashamba yao.Hongera kwa serikali yetu kwa kulivalia njuga suala la ustawi wa wananchi na juhudi za kutunza mazingira
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved