Serikali imetoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa ya Nyanda za juu kusini kuhakikisha kuwa ardhi haiwi kikwanzo kwa wawekezaji vijana pamoja na kuanzisha benki ya ardhi ambayo itatumika kuwakodishia viijana kwa mkataba maalumu.
Maelekezo hayo yametolewa na Ofisi ya waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kupitia taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Beno Malisa wakati wa ufunguzi wa sherehe za maonesho ya nanenane zinazoendelea katika viwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya leo Agost 2, 2025.
Taarifa hiyo imetoa maagizo matano kwenda kwa Wakuu wa Mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Ruvuma, Mbeya, Iringa na Njombe na kuwaelekeza kuweka mkazo katika matumizi ya bora ya ardhi, Matumizi sahihi ya viuatilifu na kemikali, Usalama wa chakula katika kaya, kutokuvuna mazao kabla ya wakati na Matumizi ya ardhi kwa wawekezaji vijana.
"Kufuatia wimbi kubwa la wawekezaji vijana, kunauhitaji wa kuwa wa ardhi ili vijana pamoja na wadau mbalimbali waweze kuwekeza katika kilimo ni vitu ambavyo haviepukiki hivyo niwaombe kwenda kusimamia halmashauri kutenga hekta 100 kwamaana ya kuwakodishia kwa mkataba maalumu na kuboresha mapato yao ama kuiweka kuwa benki ya ardhi ya uwekezaji mhakikishe ardhi haiwi kikwanzo kwa wawekezaji vijana," amesema Mhe. Malisa kwa niaba ya Mhe. Waziri Mkuu.
Maelekezo mengine ni kuweka mkazo wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ukileta maafa katika jamii, pamoja na kuingilia maeneo ya mapitio ya wanyama wa porini kama Tembo hali ambayo imekuwa ikisababisha uharibifu na usumbufu kwa binadamu hiyo wakuu wa mikoa watekeleza mpango mkakati wa matumizi bora ya ardhi vizuri.
"Tunapohamasisha matumizi ya mbolea na viuatilifu tuwaatumie vizuri maafisa ugani ili tutumie vizuri viuatilifu, mbolea na kemikali zote zinazotumika ili zisilete athari kwa bimadamu na mazingira" Ameongeza Mhe. Malisa.
Ameelekeza Tume ya umwagiliaji inapojenga miundombinu ya umwagiliaji, katika maandiko ya miradi yahusishe vichomea taka vya viuatilifu ili makasha yale yaliyowekewa dawa na viatilifu mbalimbali yakitumika bila utaratibu au vikiteketezwa katika njia isiyo nzuri italeta athari katika mazingira na inachochea mabadiliko ya tabia nchi na kutuingiza kwenye hasara.
Maelekozo mengine ni kusimamia usalama wa chakula katika ngazi ya kaya kwani haiwezekani kupitisha msako kwenye kila kaya kuona hali ya chakula lakini ni jambo mhimu na nyeti hivyo amewaomba viongozi wa dini na viongozi wa kimila kusisitiza wananchi kutunza chakula na wakihifadhi kwa matumizi ya muda mrefu ya kaya ili kuepuka wananchi kuzalisha lakini ikija njaa wanapata njaa pia.
"Nendeni mkasimamie kulima kuacha kuvuna mazao hasa ya biashara kabla ya muda wake, imekuwa ni changamoto hasa kwa mazao kama Pareto zao ambalo linatengeneza fedha nyingi za kigeni lakini kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakulima kuvuna au kukausha Pareto kabla ya wakati wake, hii inasababisha wananchi kukosa mapato ambayo wangeyapata na niwasisitize mkumbushane umuhimu wa kuvuna kwa wakati ili kufikia ubora ule unaostahili katika mazao yetu," Amehitimisha Mhe. Malisa.
Mwisho.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved