Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, ametangaza muda wa nyongeza hadi Septemba 25,2025, kuwa mwisho wa matumizi ya mkaa na kuni katika taasisi za umma na binafsi zinazohudumia watu zaidi ya 100 mkoani hapa.
Katazo hili ni muendelezo wa kampeni ya kitaifa ya kubadili matumizi ya nishati ya kupikia kutoka kuni na mkaa ambazo zimekuwa na athari hasi katika mazingira kwenda kutumia nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo leo Julai 22,2025 amesema ongezeko la muda limetokananna sababu mbalimbali ambazo ilitakiwa muda wa ziada ili ziweze kukamilika.
"Serikali imeendelea kufanya maboresho mbalimbali katika jamii hivyo kulingana na maelekezo ya serikali ilipaswa hadi kufika Januari 31,2024 taasisi zote zinazohudumia kuanzia watu kati ya 100 hadi 300 taasisi hizo zilitakiwa ziwe zimeanza kutumia nishati safi ya kupikia lakini kwa kushauriana na viongozi wengine tumeshauriana na kuona kwamba tutoe muda kidogo ili changamoto zilizokuwepo ziweze kutatulia na matumizinya nishati safi ya kupikia yaanze mara moja," amesema Mhe. Mrindoko.
Katika hatua nyingine Mhe Mrindoko amepokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya elimu mkoani hapa ambapo Afisa elimu Mkoa wa Katavi Dafroza Ndalichako amesema mkoa umepokea jumla ya bilioni 4.2 katika shule 44 kwaajili ya kutekeleza shuguli za ujenzi wa shule mpya 5 ujenzi wa vyumba vya madarasa ya elimu ya msingi matano, ujenzi wa madarasa ya mfano ya elimu ya awali 10 na ujenzi wa matundu 192 ya vyoo.
Mwisho.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved