Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko akikata utepe kuzindua Safari za Kila Jumatatu za Shirika la Ndege Nchini ATCL katika Uwanja wa Ndege Mpanda Mkoani Katavi
Na: John Mganga-IO Katavi RS
Kuanzishwa kwa ratiba mpya ya Safari za Ndege za Shirika la Ndege Nchini ATCL Siku ya Jumatatu kwa ruti ya Katavi –Dar Es Salaam ni fursa mpya kwa Wananchi wa Mkoa wa Katavi na Mikoa ya Jirani kusafiri na ndege mara 4 kwa wiki hali itakayochochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Biashara na Ukuaji wa Sekta ya Utalii, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko ameeleza.
Kwa sasa Ndege za ATCL zitafanya safari zake za Mpanda Dar Es Salaam mara Nne kwa wiki kwa siku za Jumatatu,Jumanne ,Alhamisi na Jumamosi badala ya utaratibu wa mwanzoni ambapo Ndege hizo zilikuwa zikitua mara tatu kwa wiki.
Akizindua Ratiba mpya ya Safari za Ndege za Shirika la Ndege Nchini ATCL kwa Siku ya Jumatatu, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko amelipongeza Shirika la Ndege Nchini ATCL kwa kuona umuhimu wa kuanzisha ruti ya nne ya safari za Dar-Mpanda ambapo ameeleza kuwa hatua hiyo ya kufanya Safari mara nne kwa wiki Mkoani Katavi itachochea ukuaji wa Uchumi pamoja na ukuajji wa Biashara baina ya Mikoa ya Jirani na Mkoa wa Katavi pamoja na Nchi zilizo katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Mhe.Mrindoko amesema Sekta ya Usafirishaji katika Mkoa wa Katavi imeendelea kuimarika mara dufu kutokana na Kumalizika kwa Barabara ya Mpanda Tabora ambapo kwa sasa uwepo Safari za Ndege Mara nne kwa Wiki ni kiashiria tosha kuwa Mkoa wa Katavi unapiga hatua kubwa kimaendeleo.
Aidha Mhe.Mrindoko amemshukuru Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo makubwa ambayo yamefanyika katika Mkoa wa Katavi Katika Nyanja mbalimbali.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya Utalii Mh.Mrindoko amesema kufuatia Uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour uliofanywa na Rais Samia Nchini Mkoa wa Katavi unaguswa moja kwa moja kutokana na Uwepo wa Mbuga kubwa ya Wanyama ya Katavi ambapo uwepo wa Safari za Ndege mara nne kwa wiki kunawahakikishia Watalii wanaokuja Mkoa wa Katavi kutalii kuwa wanao uwezo wa kusafiri mara nne kwa Wiki kufuatia maborsho yaliyofanywa na Shirika la Ndege Nchini ATCL.
Meneja wa Shirika la Ndege ATCL Mkoani Katavi Bw.Peter Kilawi amesema hatua ya kuongeza Safari za Ndege za Mpanda- Dar Es Salaam ni matokeo ya maoni ya wadau mbalimbali pamoja na Wasafiri wa Shirika hilo pamoja na kukidhi matakwa ya Shirika hilo kupanua wigo wa Kibiashara.
Kilawi ameeleza kuwa lengo la ATCL ni kuhakikisha kuwa Shirika la Ndege Linaendelea kuwa kichocheo cha Ukuaji wa Uchumi katika Mkoa wa Katavi na kwamba kuanzishwa kwa ratiba ya safari hiyo licha ya uwepo wa changamoto ya Mfumuko wa Bei ya Mafuta ya ndege,ni matarajio yao kuwa Safari hizo zitaleta tija kwa Shirika hilo kwa siku za Usoni.
“Leo ndiyo tumezindua safari yetu ya kwanza kwa siku ya Jumatatu na Idadi ya Abiria hairidhishi lakini kutokana na changamoto ya Mfumuko wa Bei ya Mafuta nauli zimeongzeka kwa kiasi Fulani lakini sio mbaya tunaendelea kufanya mazungumzo na Uongozi ili kuona namna gani Wasafiri watapata nafuu zaidi ya kusafiri jambo litakaloongeza Idadi ya Abiria.”Alisema Kilawi.
Jakob Timoth Mkazi wa Manispaa ya Mpanda amelishukuru Shirika la Ndege ATCL kwa kuongeza safari zake kufikia mara nne kwa wiki ambapo ameeleza kuwa hatua hiyo ni fursa kwa Mkoa wa Katavi kupiga hatua kubwa katika maendeleo hususani katika Sekta ya Biashara.
Jofrey Martin Mkazi Wa Mpanda licha ya Pongezi kwa shirika la Ndege ametoa Ushauri kwa Shirika hilo kuona haja ya kuangalia upya Nauli zao ili kutoa fursa kwa abiria wengi kutumia Usafiri huo muhimu na wa haraka.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved