• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

RC MRINDOKO AZINDUA MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA NA MAZAO MENGINE KWA MWAKA 2025/26

Posted on: June 9th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, ameongoza sherehe ya uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa pamba na mazao mengine kwa mwaka 2025/26, hafla iliyofanyika kwa katika Kijiji cha Kapalala na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, vyama vya ushirika, wakulima, na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo.

RC Mrindoko amewataka wakuu wa wilaya kuhakikisha kuwa mauzo ya mazao yote yanapitia kwenye vituo rasmi vilivyoidhinishwa na serikali pamoja na mifumo rasmi ya kibiashara. Amesisitiza kuwa utaratibu huo unasaidia kudhibiti uuzaji holela wa mazao, huku ukihakikisha wakulima wanabaki na akiba ya chakula na kuuza ziada pekee.

Ameeleza kuwa kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS), mazao ya pamba na tumbaku yanapaswa kusimamiwa kwa umakini mkubwa. Amebainisha kuwa kumekuwepo na matukio ya hujuma kutoka kwa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wanaokiuka taratibu za kilimo cha mkataba na kuingia mikataba isiyo rasmi na wakulima. Amewaelekeza wakuu wa wilaya kusimamia kwa karibu utekelezaji wa kilimo cha mkataba kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, ili kuwalinda wakulima dhidi ya unyonyaji unaofanywa na watu binafsi wanaotoa mikopo ya pembejeo kisha kujinufaisha na mazao ya wakulima.

Amefafanua kuwa mkoa wa Katavi umeungana na mikoa mingine katika kuanza kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuanzia na zao la ufuta katika msimu huu wa 2025/26. Ameeleza kuwa mfumo huo uliwahi kujaribiwa mwaka 2019/20 lakini ukakumbwa na changamoto zilizofanya utekelezaji usiendelee. Hata hivyo, kutokana na mafanikio yanayoonekana katika mikoa mingine, Katavi imeamua kurejea kwenye mfumo huo kwa lengo la kuhakikisha wakulima wananufaika kupitia usalama wa soko na ongezeko la thamani ya mazao yao.

Mwakilishi kutoka Bodi ya Pamba, Bw. Bugelaha Filbert, amesema kuwa mkulima ili aweze kufaidika na kilimo chake ni lazima azalishe kwa tija, kwa maana ya kupata mavuno mengi katika eneo dogo. Amesisitiza kuwa Bodi ya Pamba inaendelea kusisitiza matumizi ya mbolea na mbegu bora sambamba na matunzo sahihi ya zao la pamba.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • RC MRINDOKO AZINDUA MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA NA MAZAO MENGINE KWA MWAKA 2025/26

    June 09, 2025
  • RC MRINDOKO AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA KATAVI, ATOA WITO WA AMANI NA USHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025.

    June 05, 2025
  • JAJI MKUU WA TANZANIA ASISITIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA UTOAJI HAKI.

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved