RC KATAVI, TAGETI 85% UTOAJI MAJI VIJIJINI 2025 TUTAIFIKIA BILA CHENGA
Kiongozi Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko leo amekabidhi mitambo 2 ya magari ya kuchimba visima vya maji kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) kwa ajili ya mkoa wake.
Mhe. Mrindoko amesema mitambo 2 ya magari hayo imetokana na programu ya UVIKO 19 iliyotenga fedha pamoja na mambo mengine kwa ajili ya ununuzi wa mitambo ya uchimbaji wa visima vya maji.
Amesema mitambo itarahisisha utoaji wa huduma ya maji vijijini kwa sababu mkoa utakapokuwa na uhitaji wa uchimbaji wa visima hakutakuwa na shida ya upatikanaji wa vifaa.
Mhe. Mrindoko amesema seti ya mitambo ya magari hayo, iliyo na uwezo kuchimba visima hadi mita 400 kwenda chini ya ardhi, imeshachimba tayari visima 12 katika Mkoa wa Katavi kwa ajili ya wananchi wake.
Amemhakikishia mwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, aliyehudhuria hafla ya makabidhiano ya magari hayo, kuwa lengo la utoaji wa maji kwa 85% ifikapo 2025 kwa wananchi wa vijijini litafikiwa bila chenga kwa sababu mkoa umejipanga vizuri
Kisha kukabidhi mitambo hiyo, Mhe Mrindoko ameielekeza RUWASA kuitumia mitambo hiyo kwa ajili ya kuchimba visima, kukarabati na kufufua visima kwa ajili ya wananchi wake na si kwa malengo mengine.
Amewataka pia wananchi kutunza vyanzo maji na miradi ya maji iliopo ili iweze kuendelea kutoa huduma iliyokusudiwa
Maji ni kitu cha msingi sana katika maisha ya viumbe na maendeleo duniani, hatuna budi kuvitunza vyanzo vya maji na mzingira yetu ili rasilimali hii iweze kutusaidia sisi wanadamu.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved