Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akikata utepe ishara ya kuzindua zoezi la ugawaji wa pikipiki zilizotolewa na RUWASA makao makuu kwa ajili ya jumuia za watumia maji 12 Agosti 2022.
Isinde Mtapenda
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko amewataka Wananchi Mkoani Katavi kuwa walinzi wa miundombinu ya Maji pamoja na vifaa mbalimbali vinavyosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo ili kuendelea kunufaika na miradi inayojengwa na Serikali kwa ajili yao.
Mhe.Mrindoko ametoa rai hiyo akiwa Isinde Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Mtakuja/Songambele pamoja na tukio la kukabidhi piki piki 10 zilizotolewa na Wakala ya usambazaji maji na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA Makao makuu zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 32 kwa ajili ya usimamizi wa huduma za Maji katika ngazi ya Jamii.
Mhe.Mkuu wa Mkoa amewataka Wananchi kuwa walinzi wa vyombo vya usafiri vilivyotolewa kuhakikisha kuwa vinatumika kwa shughuli iliyokusudiwa ya kusimamia shughuli za upatikanaji wa Maji katika ngazi ya Jamii.
Aidha Mhe.Mrindoko amemtaka Meneja wa RUWASA Mkoa wa Katavi kuhakikisha kuwa miradi yote ambayo haikuwa imekamilika katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2021/2022 pamoja na miradi ambayo utekelezaji wake unafanyika katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 inakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kuondokana na changamoto ya uhaba wa maji katika maeneo yao.
Kwa upande wake meneja wa RUWASA Mkoa wa Katavi Bw.Peter Ngunula amesema Mkoa umepokea pikipiki hizo kutoka RUWASA makao makuu kwa ajili ya Wilaya tatu za Mlele,Tanganyika na Mpanda.
Akizungumzia kuhusu hali ya upatikanaji wa maji Mkoani Katavi Bw,Ngunula amesema hali ya upatikanaji wa maji Mkoani Katavi ni Asilimia 70 ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2021/2022 miradi iliyokuwa katika utekelezaji ilikuwa 41 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 27. ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 ruwasa Mkoa wa Katavi unatekeleza miradi 4 yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.19
Ngunula amesema kuwa kukamilika kwa miradi ya Maji inayotekelezwa kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 kutapelekea huduma ya maji kuwafikia watu wengi zaidi ambapo upatikanaji wa Maji unatarajiwa kuwa asilimia 88.
Kwa upande wao Diwani wa Kata ya Mtapenda Mhe.Eliezeli Fyula pamoja na Diwani wa Kata ya Kapalala Mhe.Lindila Matege kwa niaba ya Wananchi wameishukuru Serikali ambapo wameahidi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa miundombinu ya Maji inatunza na kulindwa.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved