RC KATAVI ATOA POLE KWA WANANCHI WALIOGUSWA NA MSIBA WA AJALI YA BASI
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amewapa pole wananchi wote walioguswa na vifo vya watu 9 vilivyotokea jana baada ya Basi la abiria kupata ajali katika eneo la Nkondwe Wilayani Tanganyika, Mkoa wa Katavi.
Mhe. Mrindoko ametoa pole hizo leo wakati akimshukuru Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi Ndugu Iddi Kimanta aliyefika ofisini kwake kumpa pole kutokana na madhila ya ajali hiyo.
Amesema ajali ya Basi hilo (kwa jina Kombas) ilitokea katika kona kali ya eneo la Nkondwe wakati Dereva wa Basi hilo aliposhindwa kukata kona hiyo na Basi kusesereka zaidi ya mita 150 na kutumbukia katika Korongo lenye urefu wa mita 75 kwenda chini.
Mhe. Mrindoko ametaja watu waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni 9 na wale waiojeruhiwa katika ajali hiyo ni watu ni 30.
Amesema hali ya majeruhi waliofikishwa katika Hospitali za Majalila, Manispaa na Hospitali ya Rufaa kwa ajili ya huduma za matibabu inaendelea vizuri ambapo majeruhi 11 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na wengine 19 bado wanaendelea na matibabu. Kwa wale wanaohitaji huduma za kibingwa tunaendelea kusimamia ili majeruhi hao na wengine wote wanapata huduma wanazostahili.
Mhe. Mrindoko amesema tunaendelea kuwaombea majeruhi kwa Mwenyezi Mungu ili awajalie uponyaji wa haraka na baadaye warejee kwenye majukumu yao.
Serikali ya Mkoa imetoa utaratibu kwa wananchi waliofiwa na ndugu zao kwenda katika Hospitali kutambua miili ya ndugu zao na kuichukua kwa ajii mazishi katika familia zao.
Leo kuanzia saa 7:00 mchana vingozi wa serikali, vyama vya siasa na wananchi wote watafanya ibada ya kuaga miili ya marehemu kwa ajiili ya mazishi kwenye familia zao.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved