Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko katika ukaguzi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika 20 Julai 2022.
Katavi-Majalila
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko ametoa Mwezi Mmoja kwa Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kuhakikisha kuwa wanakamilisha Ujenzi wa majengo ya Wodi ya Wanawake ,Wanaume na Watoto ili Wananchi waanze kupata huduma katika Hospitali hiyo.
Mhe.Mrindoko ametoa agizo hilo baada ya kutoridhishwa na kasi ya Ujenzi wa Majengo hayo yanayoendelea kujengwa katika Hospitali hiyo ambapo ameeleza kuwa kuchelewa kutumika kwa majengo hayo kunasababisha kushusha thamani ya fedha na kuathiri uteklezaji wa malengo mahsusi ya Serikali.
Aidha Mhe.Mwanamvua pamoja na maagizo aliyotoa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa maendeleo mazuri ya Ujenzi wa Jengo la ICU katika Hospitali hiyo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Daktari Alex Mrema ameeleza sababu kubwa inayoathiri kasi ya ujenzi wa baadhi ya Majengo katika Hospitali hiyo ya Wilaya kuwa ni pamoja na kuwepo kwa Mfumuko wa bei kutokana na gharama za bidhaa za Ujenzi kutoka viwandani kuwa juu,kuchelewa kufika kwa vifaa vya Ujenzi kutokana na umbali hadi kufikia eneo la Ujenzi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved