Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko ameendelea kuwasisitiza Wananchi Mkoani humo kutunza akiba ya chakula ili kuchukua tahadhari dhidi ya Ukame.
Bi.Mrindoko ametoa rai hiyo katika kikao cha Bodi ya barabara kilichoketi 23 Novemba 2022 kujadili utekelezaji wa Taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika Sekta ya Barabara.
Bi Mrindoko ameeleza kuwa kutokana na Mkoa wa Katavi kuwa miongoni mwa Mikoa Nchini iliyotabiriwa Mvua chini ya wastani ni muhimu kwa Wananchi Mkoani humo kuchukua tahadhari kwa kutunza akiba ya chakula sambamba na kupanda mbegu zinazokua ndani ya muda mfupi.
Aidha amewataka Wananchi kuzingatia utaratibu wa kujisajili kupata namba maalumu ya utambulisho ili iwe rahisi Wananchi hao kupata mbolea ya ruzuku hatua itakayosaidia Wananchi hao kulima kilimo cha kisasa cha kutumia mbolea.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved