Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akikabidhi pikipiki kwa mmoja wa Maafisa Tarafa Mkoani Katavi Leah Gawaza,Afisa Tarafa kutoka Tarafa ya Misunkumilo wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 8 kwa Maafisa Tarafa Mkoani Katavi 13 Januari 2022.
Na:OMM- Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko leo 13 Januari 2023 amekabidhi Pikipiki 8 kwa Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Katavi zenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 40 kama vitendea kazi ili kurahisisha Utekelezaji wamajukumu mbalimbali kwa Maafisa hao.
Akizungumza wakati wa kugawa pikipiki hizo Mkuu wa Mkoa Mrindoko amewataka Maafisa Tarafa waliokabidhiwa pikipiki hizo kutumia vyombo hivyo vya usafiri kwa shughuli zilizokusudiwa ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali zikiwemo maagizo mbalimbali ya Serikali.
Amewataka Maafisa Tarafa kutumia vyombo hivyo vya Usafiri kufanya ufuatiliaji wa karibu wa Mwenendo wa Wanafunzi kuripoti Mashuleni katika kipindi hiki cha kuanza muhula wa Masomo 2023 kwa kidato cha kwanza pamoja na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa uandikishaji Wanafunzi wa Darasa la kwanza katika mhula wa mMsoko 2023.
Aidha amewasisitiza Maafisa Tarafa hao kufanya ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha kuwa mbole ya ruzuku inagawiwa kwa Wananchi pamoja na kuhakikisha kuwa Maafisa Ugani wanatimiza wajibu wao katika utoaji elimu kwa Wananchi kuhusu kilimo cha kisasa.
Awali Katibu tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa ameeleza lengo la Serikali Mkoani Katavi kutoa pikipiki hizo kwa Maafisa Tarafa ni kuhakikisha Maafisa hao wanatekeleza majukumu yao kikamilifu hasa katika kipindi hiki cha msimu wa Kilimo ambapo Maafisa hao wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa mbolea ya Ruzuku inawafikia Wananchi ipasavyo pamoja na kusimamia ufuatiliaji wa Wanafunzi kuripoti shuleni kwa ajili ya kuanza Masomo.
“Hiki tunachokifanya leo ni Matokeo ya mpango wa Mkoa ambapo katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 Mkoa ulitenga Jumla ya Shilingi Milioni Arobaini na Nne na Laki nne na Elfu Arobaini kwa ajili ya Ununuzi wa Pikipiki.Mkoa wa Katavi unazo Tarafa 10 sasa kutokana na mabadiliko ya Bei tumepata Pikipiki 8 kwa ajili ya Kata Nane ambazo ni Kashaulili,NsimboMisunkumilo,Kabungu,Mwese,Inyonga,Karema,Mamba, na Inyonga ambapo kwa Tarafa za Mpimbwe na Ndurumo zitanunuliwa katika mwaka ujao wa Fedha”Alisema Katibu Tawala Rugwa.
Baadhi ya Maafisa Tarafa waliokabidhiwa pikipiki hizo wameishukuru Serikali kwa kujenga mazingira wezeshi ya kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo ambapo wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuwatumikia Wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa nguvu zote.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved