RC KATAVI AHADI MAZINGIRA RAFIKI KWA WAWEKEZAJI
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amefanya ziara ya kikazi katika migodi mbali mbali ili kujionea hali halisi ya uendeshaji wa migodi hiyo katika mkoa wake.
Katika ziara hiyo Mhe. Mrindoko ametembelea migodi ya Kampuni ya Mgodi ya Katavi, Jieng China Company na Awa Group iliyopo katika Halmashauri ya Nsimbo na Manispaa ya Mpanda, Wilaya ya Mpanda.
Mhe. Mrindoko amewahakikishia wawekezaji hao kuwa serikali itaendeleea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wote ili kuwawezesha kufanya kazi zao vizuri na kuvutia wawekezaji wengi zaidi kuwekeza katika mkoa wake
Mhe. Mrindoko amezipongeza Kampuni hizo kwa kushiriki katika ujenzi wa taifa la Tanzania kwa kulipa tozo za serikali, kutengeneza ajira kwa vijana na ujenzi wa miundombinu ya kijamii mfano shule na vituo vya polisi katika Wilaya Mpanda
Amesema serikali itashirikiana na kila mwekezaji katika uendeshaji wa sekta ya madini katika mkoa wake hasa kujenga mazingara ya amani na usalama na utatuzi wa changamoto mbali mbali mfano umeme, barabara na migogoro mbali mbali ya kijamii.
Mkoa wa Katavi umejaliwa madini ya aina nyingi(dhahabu, shaba, silver) na sekta ya madini mkoani humo inatoa mchango mkubwa sana katika pato la taifa na ustawi wa wananchi wa mkoa huo.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved