Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko 27Juni 2022 akizungumza wakati wa Baraza la Hoja Manispaa ya Mpanda.
Na:John Mganga-Katavi RS
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrondoko ametoa siku 35 kwa kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya Watumishi watakaobainika kuhusika na kutokuwasilisha fedha zilizokusanywa kupitia mfumo wa Mapato bila kuziwasilisha benki.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo katika baraza la Madiwani la Manispaa ya Mpanda lililoketi kupitia na kujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali CAG.
Mkuu wa mkoa ameeleza kuwa ipo changamoto ya usimamizi mbovu wa Mashine za kukusanyia mapato jambo linalochangia kuzalisha wadaiwa wengi katika mfumo wa mapato akitolea mfano Shilingi Milioni 33.4 ambazo zinasomeka kwenye mfumo licha ya wakusanyaji kupewa bili ili kuziwasilisha fedha hizo Benki.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Bi.Sophia Kumbuli amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo ameahidi kuchukua hatua stahiki kwa wale wote wanaohusika kusababisha changamoto hiyo ya deni la shilingi Milioni 33.4 ambalo linasomeka katika Mfumo wa kukusanyia mapato LGRCIS.
Aidha Mhe.Mrindoko ameutaka uongozi wa Manispaa ya Mpanda kuhakikisha kuwa inashughulikia na kumaliza kabisa hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kuhakikisha kuwa hoja hizo hazijirudii tena.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved