• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

RAS MSOVELA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE.

Posted on: June 19th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Albert Msovela, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa hatua ya kujibu na kutekeleza kwa weredi maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

Akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi tarehe 19 Juni, 2025 kwa ajili ya kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na maagizo ya LAAC, Katibu Tawala amesema Halmashauri ya Nsimbo imekuwa kinara katika utekelezaji wa maagizo hayo kwa wakati, jambo linaloonesha uwajibikaji na utayari wa kuzingatia misingi ya utawala bora.

RAS Msovela Ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa hoja, hatua zilizochukuliwa na halmashauri hiyo zinaonesha kuwa hoja hizo zingeweza kuepukwa endapo majibu yangewasilishwa kwa wakati, kwa ufasaha, na kwa vielelezo kamili. Hata hivyo, amesisitiza kuwa msingi wa mafanikio hayo unatokana na watumishi wa halmashauri hiyo kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya kazi, na hivyo kuna matarajio kuwa hoja zote zilizobaki zitapatiwa majibu sahihi kwa wakati.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa na Mkaguzi wa Ndani, Bw. Chambi Ngelela, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ilipokea hati inayoridhisha (Unqualified Opinion) kutoka kwa CAG. Taarifa hiyo imeeleza kuwa jumla ya hoja 19 kati ya zilizowasilishwa zimefungwa baada ya kupatiwa majibu ya kuridhisha, huku hoja 40 zikiwa bado hazijafungwa. Aidha, maagizo yote 6 yaliyotolewa na Kamati ya LAAC yamekamilika kutekelezwa.

Akihitimisha kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo, Mhe. Halawa Charles Malendeja, amesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano wa karibu uliopo kati ya wataalamu wa halmashauri hiyo na viongozi wa kisiasa, jambo ambalo limeiwezesha halmashauri kusimamia vyema utekelezaji wa mipango na majukumu yake katika kipindi cha miaka mitano.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • BARAZA MAALUM LA MADIWANI TANGANYIKA LAJADILI TAARIFA YA CAG, WATUMISHI WATAKIWA KUFUATA SHERIA.

    June 17, 2025
  • RAS MSOVELA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE.

    June 19, 2025
  • MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO AFRIKA, CHAGULAGA BADO NI KILIO KWA WASICHANA KATAVI.

    June 16, 2025
  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved