RC KATAVI APIGA STOP UNYANYASAJI SEHEMU ZA KAZI
Kazi ni sehemu ya asili ya binadamu wote duniani. Kazi ni maendeleo; humletea heshima na shibe mtu nyumbani kwake, husaidia mwili kuwa na afya njema.
Kazi huondoa fedheha, umaskini na ukoloni mamboleo. Kazi ina manufaa makubwa kwa mwanadamu, binadamu wote duniani hatuna budi kuithamini na kuiheshimu kazi.
Mataifa yote duniani yanaheshimu na kutahamini kazi kwa sababu huleta maendeleo katika mataifa na katika maisha ya mwanadamu.
Nchini Tanzania , tuliazimia kufanya kazi ili kujiletea maendeleo mara baada ya kupata uhuru wetu. Tulihamasishana, uhuru bila kazi hauna maana katika maisha yetu, kama taifa lazima tufanye kazi.
Karibu miongo 6 ya uhuru wetu kama taifa, Tanzania tumepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kutokana na kufanya kazi. Tuna vituo vingi vya kutolea afya, tuna dawa na vifaa tiba katika hospitali zetu, tuna mtandao mkubwa wa barabara, madaraja, viwanja vya ndege na bandari, tuna miundombinu ya elimu na vifaa mbali mbali vya kufundishia katika shule zetu. Tuna mambo mengi ya kimaendeleo katika nchi yetu.
Katika Mkoa wa Katavi tunajivunia maendeleo lukuki. Kwa kutaja machache, tuna hospitali na vituo vya kutolea huduma ya afya kwa wananchi wetu, tuna bandari, tuna kiwanja cha ndege, tuna barabara na bandari, tuna chakula cha kutosha kwa wananchi wetu.
Bidii na maarifa ya kazi kwa wafanyakazi wa umma, sekta binafsi kwa kushirikiana na wananchi wa Mkoa wa Katavi umepata maendeleo makubwa katika sekta mbali mbali.
Katika maadhimisho ya kumbukizi ya Siku ya wafanyakazi duniani, yaliyoadhimishwa kimkoa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili, Mjini Mpanda, Kiongozi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko, kwa dhati ya moyo wake, hakusta kuwapongeza wafanyakazi wote katika mkoa wake kwa kazi nzuri waliyofanya katika kuwahudumia wananchi wa mkoa huo.
Mhe. Mrindoko amewataarifu wafanyakazi kuwa kazi wanazozifanya katika mkoa wake ndizo ambazo zimeleta mafanikio makubwa na kuuheshimisha mkoa.
Amebainisha kazi hizo kuwa ni pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM, utoaji wa huduma na utatuzi wa kero mbali mbali kwa wananchi.
Kiongozi huyo, amewasihi wanafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa, nidhamu ya hali ya juu, kujituma na kutumia muda wao vizuri katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa mkoa wake.
Amewaahidi wafanyakazi hao kuwa serikali ya mkoa wake itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kazi kwa wafanyakazi wote ili kuwezesha mipango, programu na miradi ya maendeleo kusonga mbele zaidi.
Amewaonya waajiri wote katika mkoa wake kutojihusisha na unyanyasaji wa wafanyakzi wao, kudumisha staha sehemu za kazi, nidhamu na kuwathamini na kuwaheshimu wafanyakazi wote kwa mujibu wa Sheria, Kanununi, Taratibu, Miongozo, Mila na Desturi za kitanzania.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved