Katibu tawala Mkoa wa Katavi Albert Msovela amesema ni lazima watumishi wa umma kuzingatia maadili na miiko ya kazi kwa mujibu wa sheria kwani baadhi ya watumishi wamekuwa na changamoto nyingi ambazo hazikwepeki zinazosababishwa na mambo ambayo si ya kiutumishi ikiwemo ubadhirifu na Rushwa.
Ameyabainisha hayo wakati akifungua mafunzo ya kamati za kudhibiti uadilifu mahali pa kazi ambayo yanazihusu Halmshauri za mikoa mitatu ambayo ni Kigoma, Rukwa, na Katavi yanayoendelea katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Katavi leo Aug 26, 2025 ambapo amewataka wajumbe kutumia nafasi hiyo kutambua kuwa kunachangamoto ambazo zinahitaji ufumbuzi wa haraka kwa baadhi ya watumishi.
"Tunachangamoto nyingi ambazo hazikwepeki zinazosababishwa na mambo mengine ambayo si ya kiutumishi ikiwemo ubadhirifu na Rushwa, Matarajio yangu kupitia mafunzo haya na mfumo huu wa maboresho mnaoenda kufundishwa itakuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko katika utendaji," Amesema Ras Msovela.
Aidha ameongeza kuwa Mikakati na maadhimio ya kikao hicho yafanyiwe kazi kwa wakati kwani kumekuwa na ucheleweshaji wa utoaji wa taarifa kwenye dawati la maboresho hivyo imani ni kuwa watatumia muda vizuri na kushauriana kuhusu utendaji wa kamati hizo.
Awali akitoa taarifa ya mafunzo hayo Mratibu wa mafunzo ameeleza kuwa mafunzo yamewalenga maafisa 60 kutoka idara na vitengo mbalimbali katika tawala za mikoa na serikali za mitaa ambayo yatatolewa kwa siku mbili kisha kutengeneza maadhimio ya pamoja katika mkakati watakao uweka.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved