Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Onesmo Buswelu, amewahimiza wahitimu wa jeshi la akiba kuendeleza moyo wa uzalendo na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo watakaporejea kwenye jamii zao.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo kwa vijana 155 wa jeshi la akiba yaliyodumu kwa muda wa wiki 18 katika vituo vya Katuma na Kapanga, Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Buswelu alisema taifa linahitaji wananchi wachapakazi na wenye kujitoa kwa manufaa ya wote.
Vilevile, amewakumbusha wananchi kuhusu Uchaguzi Mkuu unaopangwa kufanyika Oktoba 29, akiwataka kushiriki kwa wingi ili kuwachagua viongozi waadilifu watakaosimamia rasilimali za taifa kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya mwaka 2050.
Ameongeza kuwa ni wajibu wa wananchi kudumisha utulivu na mshikamano wa kitaifa, huku akiwataka wagombea kuendesha kampeni kwa amani na kufuata taratibu za kisheria.
Kwa upande wao, wahitimu wametoa shukrani kwa serikali kwa mafunzo na ujuzi walioupata, wakiahidi kuendelea kulinda taifa na kuishi kwa misingi ya uzalendo. Pia wameomba kupewa nafasi zaidi za ajira, ikiwemo nafasi za VGS na fursa ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved