• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Madiwani Urambo wakoshwa na Biashara ya Hewa Ukaa Katavi.

Posted on: November 17th, 2022

Madiwani Urambo  wakoshwa na Biashara ya Hewa Ukaa Katavi

Diwani Urambo: “Tuna Misitu lakini hatujui kuitumia”

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kutoka Mkoani Tabora wamefurahishwa kwa  namna ambavyo Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi  wamenufaika kupitia Mradi wa Uvunaji wa Hewa Ukaa katika Misitu inayomilikiwa na  Vijiji pamoja  na Halmashauri Wilayani humo

Timu ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo   ikijumuisha madiwani 24 pamoja na Wataalamu 10 wamefanya ziara Mkoani Katavi Wilayani Tanganyika 16 Novemba 2022 kwa lengo la  kujifunza namna ambavyo Halmashauri imetekeleza na kunufaika na Biashara ya hewa ukaa.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kituo  cha kutolea huduma za Afya, katika Kijiji cha Kagunga,moja kati ya miradi inayotekelezwa kwa Fedha zitokanazo na uvunaji wa hewa ukaa Wilayani Tanganyika  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bw.Adam Malunkwi amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza ili kutanua wigo wa kukusanyaji wa mapato.

“Tumefika hapa kwenu kwa maana ya kuja kujifunza,Ziara yetu imekuwa yenye  mafanikio  ya kutosha kwa sababu tumejionea kwa macho.Tumeshapewa darasa zuri sana kule Wilayani  tumefundishwa,tumeelewa na hapa tumejionea kwa macho namna ambavyo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imenufaika kupitia Biashara ya Hewa Ukaa Hongereni sana. Kilichobaki hapa ni kutekeleza kwa vitendo kile ambacho tumejifunza ”Alisema Mwenyekiti Malunkwi.

Athmani Ali Mwinyiko mmoja wa Madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo amesema ni muhimu kwa Wananchi Wilayani Tanganyika kuendelea kutunza misitu ili kuendelea kunufaika na Biashara ya Hewa Ukaa.

“Bahati nzuri wameanza  hatua ya chini na sasa wamepiga hatua kubwa. Kama Halmashauri imefanikiwa kupata zaidi ya Bilioni 4 kwa mwaka kupitia mradi mmoja wa hewa ukaa, ukijumlisha na miradi mingine maana yake mapato yatakua juu zaidi ukilinganisha na Halmashauri zingine ambazo hukusanya mapato chini ya Bilioni 1” alisema Diwani Mwinyiko.

Naye Diwani Kamende wa Viti Maalumu kutoka Tabora amesema wataitumia vyema elimu waliyoipata kuanzisha Biashara ya Hewa ukaa kwa kuwa Wilaya ya urambo imebarikiwa kuwa na Misitu ya kutosha.

“Wilaya ya Urambo tuna misitu mizuri lakini hatuifanyii kazi maana mnaweza mkawa na kitu lakini hamjui kukitumia,tumeona namna wanavyonufaika na Hewa ukaa na sisi niahidi tutaifanyia kazi Elimu hii na  tutawazidi hadi walimu”.Alisema Diwani huyo kutoka Uyombo huko Urambo.

Awali akiwasilisha mada ya mradi wa hewa ukaa  Mkuu wa Kitengo cha Maliasili Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Bruno Mwaisaka amewaambia Madiwani na Wataalamu kutoka Urambo kuwa ili waweze kunufaika na Biashara ya Hewa Ukaa ni muhimu kujipanga vyema kutunza Misitu pamoja na kuimarisha ulizi dhidi ya Wavamizi mbalimbali ikiwemo Majangili.

Ameongeza kuwa ni muhimu kuzingatia muongozo wa Kitaifa wa uanzishaji wa Biashara hiyo ya hewa ukaa na pia kuwa makini katika uandfaaji wa mikataba ya Biashara hiyo ili iweze kuleta manufaa zaidi kwao.

Biashara ya hewa ukaa Wilayani Tanganyika ilianza mwaka 2018 ukiendeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ,Taasisi ya CARBON Tanzania kwa kushirikiana na mradi wa Tuungane kwa Afya na Mazingira bora ukitekelezwa katika jumla ya Vijiji nane ambavyo ni Lugonesi,Mwese,Lwega,Bujombe,Kapanga,Katuma,Mpembe, na Kijiji cha Kagunga.

Aidha mradi huo unahusisha Misitu ya Vijiji yenye ukubwa wa Hekta 216,944 za Ardhi katika Vijiji vyote  ambapo  wakazi zaidi ya 34,242 wamefaidika na mradi katika sekta za Afya Elimu,na kuwezesha vikundi vya ujasiriamali.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MRINDOKO AZINDUA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU (GAWE) 2025

    May 05, 2025
  • RC MRINDOKO AIHAKIKISHIA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI USALAMA WA UCHAGUZI MKOANI KATAVI.

    April 29, 2025
  • WAZIRI NDEJEMBI AONGOZA MIKAKATI YA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI ENEO LA WESTERN, KITONGOJI CHA LUHAFWE – H/ WILAYA YA TANGANYIKA

    April 24, 2025
  • PPPC WATOA ELIMU UIBUAJI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA UBIA.

    April 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved