Na: Mwandishi wetu.
Kuimarika mara dufu kwa miundombinu ya uchukuzi Mkoani Katavi kumechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi pamoja na Mkoa huo kuendelea kuwa kitovu cha uzalishaji na kujitosheleza kwa chakula Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Hoza Mrindoko ameeleza.
Bi Mrindoko ameyasema hayo katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichoketi 23 Novemba 2022 katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Ujenzi wa Miundombinu ya barabara Mkoani humo.
Amesema kuimarika kwa miundombinu mbalimbali ya uchukuzi ikiwemo Barabara za Miji na Vijijini kumerahisisha shughuli za uchukuzi ikiwemo uingizaji wa pembejeo mbalimbali za kilimo kwa wakati pamoja na usafirishaji wa Mazao ya chakula hali inayosaidia kwa kiasi kikubwa kukuza sekta ya Uzalishaji.
Kutokana na Serikali kuwekeza fedha nyingi katika Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Barabara Mkuu huyo wa Mkoa amewataka Watumishi wa Umma Mkoani humo kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kuhakikisha kuwa adhma ya Serikali kuboresha miundombinu ili kuinua uchumi wa Wananchi inatimia.
Amesisitiza Watumishi wa Umma kushirikiana vyema na Wabunge Mkoani humo kutatua changamoto chache zilizopo katika Sekta ya Barabara pamoja na sekta zingine ndani ya Mkoa hatua itakayoharakisha utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved