• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani Kitaifa Mkoani Katavi, RC Katavi ahimiza Wadau/Wananchi kushiriki kikamilifu.

Posted on: May 13th, 2022

Na:John Mganga-IO Katavi RS.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Hozza Mrindoko ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Misitu na Nyuki pamoja na Wananchi Mkoani Katavi Kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani  kuanzia tarehe 19 hadi 21 Mwezi Mei Mwaka 2022.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake 13 Mei 2022, Mh.Mrindoko amesema Mkoa wa Katavi umepewa heshima kubwa ya kuwa Mwenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani Kitaifa ambapo Mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii,Ofisi ya Rais TAMISEMI,pamoja na   Wadau mbalimbali wapo  katika maandalizi ya  maadhimisho ya Siku ya Ufugaji Nyuki Duniani Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Azimio uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na kupambwa na Kaulimbiu inayosema Nyuki ni Uchumi,Tuwalinde na Kuhifadhi Mazingira yao”.

Ameeleza kuwa Maadhimisho haya Kitaifa yanafanyika Katavi kutokana na mchango wa sekta ya nyuki katika kukuza uchumi wa mkoa na wananchi kwa ujumla na kwamba  mdudu nyuki amekuwa na mchango mkubwa katika uchavushaji wa mimea hali inayopelekea Mkoa wa Katavi  kuendelea kubaki  miongoni mwa mikoa inayojitosheleza kwenye chakula sambamba nakuzalisha chakula cha ziada kwa mikoa mingine.

Mh.Mrindoko amesema Lengo Kuu la maadhimisho hayo ni kuwaleta pamoja  wataalam wa Nyuki, wafugaji wa Nyuki, wajasiriamali wa mazao ya Nyuki na wadau mbalimbali wa Nyuki kwa lengo la kujengeana uwezo wa namna bora ya kuendeleza Sekta ya Nyuki katika mkoa wa Katavi, Mikoa ya Kanda ya Magharibi na Nchini kwa ujumla.

Akizungumza kuhusu hali ya uzalishaji wa Mazao yatokanayo na Nyuki pamoja na faida zake Mh.Mrindoko amesema Katika kipindi cha miaka mitano (2016-2021) Mkoa wa Katavi umeshuhudia Sekta ya Ufugaji Nyuki ikiingiza kiasi cha Tsh. 13,440,900,000/= na Tsh. 4,047,984,500/= zilizotokana na lita 2,688,180 za asali na kilo 578,284 za Nta mtawalia.

Amesema  Katika kipindi hicho, Mkoa pia umeshuhudia ongezeko la takwimu za ufugaji Nyuki katika nyanja tofauti, ambapo uzalishaji wa asali umeongezeka kutoka lita 387,431 mwaka 2016 mpaka lita 496,229 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 28. Uzalishaji wa Nta nao pia umeongezeka kutoka kilo 100,086 mwaka 2016 mpaka kilo 119,009 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 19.

Ratiba ya Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani inatarajia kuanza tarehe 19 - 21/05/2022 wageni watapata fursa ya Kubadilishana mawazo juu ya uboreshaji wa sekta ya Nyuki na pia  watapata nafasi ya kujenga uelewa wa umuhimu wa Sekta ya Nyuki kupitia kongamano ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa. Miongoni mwa mada hizo ni ‘‘Athari za Mabadiliko ya tabia nchi kwenye shughuli za ufugaji nyuki’’ na ‘‘Fursa ya utalii wa nyuki na mchango wake katika uchumi’’

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MRINDOKO AZINDUA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU (GAWE) 2025

    May 05, 2025
  • RC MRINDOKO AIHAKIKISHIA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI USALAMA WA UCHAGUZI MKOANI KATAVI.

    April 29, 2025
  • WAZIRI NDEJEMBI AONGOZA MIKAKATI YA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI ENEO LA WESTERN, KITONGOJI CHA LUHAFWE – H/ WILAYA YA TANGANYIKA

    April 24, 2025
  • PPPC WATOA ELIMU UIBUAJI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA UBIA.

    April 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved