Pichani:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi katika Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane katika Viwanjwa vya John Mwakangare jijijiini Mbeya 8 Agosti 2022.
Kutoka Viwanja vya John Mwakangare Jijini Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewaagiza wakuu wa Mikoa yote Nchini kutenga Maeneo yatakayoyumika kwa ajili ya Kilimo cha mazao yanayozalishwa katika mikoa husika.
Mhe.Rais Samia ametoa agizo hilo alipohutubia kwenye kilele cha cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangare jijini Mbeya ambapo amewataka wakulima kutumia maeneo yatakayotengwa kuzalisha kibiashara ili kujitosheleza kwa chakula na kuuza katika Nchi jirani.
Aidha Mhe.Rais Samia amewataka wakulima kote Nchini kujisajili ili kupata vitambulisho ambavyo vitatumika kupata ruzuku ya mbolea kuendana na kila Msimu wa Kilimo.
Mhe.Rais Samia pia amemuagiza Waziri wa Mifugo na Uvuvi kushirikiana na Chuo cha Kilimo( SUA )kuwajengea uwezo vijana wanaohitimu katika chuo hicho ili waweze kujiajiri katika Sekta ya Kilimo.
Katika hatua nyingine Mhe.Rais ameitaka Wizara ya Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufuta Leseni za vitalu vya ranchi vilivyokodishwa nan a kujua mapato yatokanayo na Vitalu hivyo.
Aidha Rais Samia ameitaka bodi ya wakurugenzi na Ugongozi NARCO kufanya uchambuzi wa vitalu vya Ranchi vilivyokodishwa na kujua mapato yatokanayo na vitalu hivyo.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved