MKUU WA MKOA WA KATAVI AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI
Leo Jumamosi April 14,2018,Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali (Mst) Raphael Muhuga amefanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Azimio Mjini Mpanda kusikiliza kero za wananchi.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Katavi aliyekuwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa,Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Mpanda, Mlele, Nsimbo, Mpimbwe, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za umma zilizopo Mkoa wa Katavi na Wakuu wa Idara wote kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda. Mkuu wa Mkoa wa Katavi alisikiliza kero za wananchi walizowasilisha mbele yake, kisha walalamikaji walipata fursa ya kuwasilisha kero zao mbele ya Dawati la Malalamiko la Mkoa kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu katika maandishi na kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa kero hizo za wananchi zinazohitaji majibu ya haraka.
Miongoni mwa kero zilizoibuka eneo la mkutano huo ni pamoja na kero za ardhi ambapo wananchi walieleza kutoridhishwa na namna ardhi inavyotolewa na jinsi migogoro ya ardhi inavyotatuliwa.
Wananchi pia waliwalalamikia askari wa kampuni binafsi katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambao kwa kiasi kikubwa wameonekana kutokujali shida za dharula kwa wananchi wanaohitajika kupeleka dawa na chakula kwa wagonjwa waliolazwa.
Pia, amewataka watumishi wa umma katika Mkoa wake kuzingatia maadili yao ya kazi katika kuwatumikia wananchi huku akiwasisitiza kutatua kero za wananchi kwa wakati. Mkuu wa Mkoa ameahidi kuitisha tena Mkutano wa hadhara mwezi wa tano kwa ajili ya kujibu hoja zilizotolewa. Jumla ya Hoja 97 zilitolewa na wananchi hao huku hoja nyingi zikiwa ni hoja za Idara ya Ardhi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved