Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapunduzi CCM Mkoa wa Katavi imetembele kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, na kuridhishwa na kasi kubwa ya maendeleo ya miradi hiyo.
Kamati hiyo iliyoambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Ndg. Iddy Kimanta, viongozi mbalimbali wa CCM, wataalam wa kada tofauti tofauti na watumishi wa Halmashauri.
Katika ziara hiyo ilitembelea miradi ya ujenzi wa barabara ya Ifinsi-Bugwe yenye urefu wa km 21 kwa kiwango cha changarawe, Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Msingi Ifinsi, Ujenzi wa Shule Mpya ya Kamsenga, Ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya lami inayoanzia Vikonge kwenda Kigoma na Ujenzi wa Bweni la wasichana shule ya sekondari Majalila.
Ziara hiyo ilitamatika kwa Ndg. Kimanta kutoa maagizo ya ukamilishwaji wa miradi ambayo bado haijakamilika kwa muda muafaka.
“Nipongeze sana kwa H/W ya Tanganyika miradi yote inaendelea vizuri na naomba muendeleze juhudi hizi” Mhe Kimanta-M/kiti wa CCM Mkoa wa Katavi.
Aidha Chama cha Mapinduzi CCM kimetoa maagizo kwa H/W ya Tanganyika kujenga utamaduni wa kutembelea miradi ikiwemo ukamilishaji wa kuezeka majengo ya madarasa manne shule ya Msingi Ifinsi.
“Naomba mjenge utamaduni wa kutembelea miradi mara kwa mara ili kubaini mapungufu na kurekebisha. Kamsenga Mhe Rais Dkt Samia ameleta Sh Mil 600, hizi kamati za ujenzi wajengewe uwezo wa kusimamia miradi”
“Lakini pia maagizo ya chama yale madarasa manne ya shule ya msingi Ifinsi, mpaka kufikia Februari 2025 yawe yameshafunikwa na bati, tuthamini nguvu ya wananchi wanaoanzisha miradi hii” Ndg. Kimanta, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Katavi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved