Wakazi wa Mkoa wa Katavi kwa mara ya kwanza wamejitokeza kushiriki mashindano ya mbio za riadha za kilometa 20, kilometa 10, 5, 3 na 1 zinazojulikana kwa jina la Homera Marathon 2019 kwa lengo la kuchangia fedha za ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi inayokabiliwa na uchakavu mkubwa.
Mbio hizo zimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Homera ambaye amewataka wakazi wa Mkoa huo kuchangia hospitali hiyo
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wameeleza dhana nzima ya mbio hizo kuwa ni pamoja na kuimarisha afya, kuboresha miundombinu ya hospitali ya Mkoa wa Katavi.
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo sasa inatumika kama Hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Katavi ilijengwa tangu mwaka 1957.
Lengo la lililowekwa ni kukusanya shilingi milioni 194, lengo hilo lilivukwa kwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 250 ikiwa ni fedha taslimu na ahadi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved