Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Wilayani Mlele Mkoani Katavi imeibuka kidedea kwenye masuala ya Kilimo na ufugaji na kutangazwa Mshindi wa kwanza Kitaifa jijin Mbeya.
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele inazalisha kwa wingi mazaombalimbali ya chakula ikiwemo mahindi na mpunga yanayouzwa ndani nan je ya Nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Bi.Theresia Irafay amesema hatua ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kutangazwa Mshindi kunatia hamasa kwa Halmashauri hiyo ambapo ameahidi kuendelea kuhamasisha wakulima kuendelea kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula pamoja na ufugaji wenye tija wa kumkwamua Mwananchi.
Aidha Halmashauri hiyo imetoa mfugaji bora Kitafia Bw.Gabriel Nnyambi ambae ametunukiwa cheti pamoja na fedha Taslimu shilingi Milioni Nane.
Jumla ya Halmashauri tano za Mkoa wa Katavi zimeshiriki katika maonyesho ya Bidhaa za Kilimo nanenane Kikanda katika Viwanja vya John Mwakangare jijini Mbeya.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved