Kikao cha tathmini ya robo ya kwanza ya mwaka, Julai–Septemba 2025, kilichohusisha Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Lishe, na Waratibu wa Mama na Mtoto kutoka kila halmashauri, pamoja na Waganga Wakuu wa Wilaya, kimefanyika leo, tarehe 08 Oktoba 2025, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Washiriki wamejadili utekelezaji wa shughuli za kijamii, mafanikio na changamoto zilizojitokeza, sambamba na kupanga mikakati ya kuboresha huduma kwa watoto.
Mada kuu iliyojadiliwa: Elimu Jumuishi, ikisisitiza kuwa elimu jumuishi siyo tu kuwajumuisha watoto wenye ulemavu pekee, bali ni kuhakikisha kila mtoto anapata fursa sawa ya kujifunza na kustawi.
Aidha, kikao kimeangazia utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, ambapo washiriki wamesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta za afya, elimu, lishe, na ustawi wa jamii ili kukuza maendeleo bora ya mtoto.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved