• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Zoezi la Sensa kufanikiwa kwa Asilimia 100 Katavi. RC Katavi apongeza maandalizi,Asisitiza Wananchi kutoa Taarifa sahihi.

Posted on: August 24th, 2022

Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akishiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi nyumbani kwake mara baada ya Karani wa Sensa kufika kwa ajili ya zoezi hilo 23 Agosti 2022.

Mpanda-Katavi 

Zoezi la Sensa ya watu na makazi lililoanza rasmi Tarehe 23 Agusti 2022 limeendelea kupokelewa kwa muitikio mkubwa na Wananchi Mkoani Katavi huku viongozi mbalimbali wa Kimkoa na Wilaya wakiwaongoza Wananchi kushiriki Sensa katika maeneo yao.

Zoezi la Sensa ya watu na makazi Mkoani Katavi lilianza kutekelezwa saa Sita usiku ambapo makarani wa Sensa walipita katika maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko kama vile Vituo vya Mabasi,Kumbi za Starehe,Nyumba za Kulala wageni,Magereza,Polisi pamoja na baadhi ya Kaya ambapo katika maeneo hayo kumekuwa na muitikio mkubwa na utayari wa Wananchi kuhesabiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko aliwaongoza Wananchi  Mkoani humo kuhesabiwa ambapo karani wa Sensa alifika nyumbani kwake majira ya Saa 3:00 asubuhi na kuanza kutekeleza zoezi hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kushiriki Sensa Mhe.Mrindoko amesema zoezi hilo limefanyika kwa utulivu mkubwa pasi kuwepo na changamoto yoyote.

Amewashukuru wadau mbalimbali walioshiriki kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi Mkoani Katavi ambapo 

Mhe.Mrindoko  amewataka Wananchi Mkoani humo kutoa ushirikiano kwa viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuacha Taarifa sahihi kwa watakaobaki katika kaya ili kurahisisha shughuli za ujazaji wa madodoso kwa makarani wa sensa katika Kaya zao.

Aidha amesisitiza utoaji wa taarifa sahihi kwa makarani wa Sensa ili kuiwezesha Serikali kuwa na taarifa sahihi zitakazowezesha kupanga Mipango mbalimbali ya maendeleo

Mhe.Mrindoko pia ametembelea baadhi ya Kaya katika manispaa ya Mpanda kwa lengo la kujiridhisha namna ambavyo zoezi hilo la Sensa linatekelezwa katika maeneo mbalimbali ambapo pia amekutana na kuzungumza na Wafanyabiashara katika soko kuula Mpanda ambapo alitoa elimu kuhusu Sensa kwa Wananchi hao.

Kwa Upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa baada ya kushiriki kuhesabiwa amesema zoezi hilo litafanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuwa maandalizi yalifanyika kwa asilimia 100.

Nao Wananchi mbalimbali walioshiriki kuhesabiwa wameipongeza Serikali kwa maboresho ya zoezi la Sensa amnbapo kwa sasa wameshuhudia zoezi hilo likidodosa taarifa nyingi zaidi kwa kutumia TEHAMA.


MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA 

 

Picha 1;Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa akishiriki zoezi la kuhesabiwa  nyumbani kwake saa chache baada ya kuanza zoezi la Sensa ya watu na makazi 23 Agosti 2022 linaoendelea Nchi Nzima .


Picha2;Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Comredi Dkt.Beda Katani alipomtembelea nyumbani kwake wakati wa zoezi la Sensa ya watu na makazi Siku ya 23 Agosti 2022 saa chache baada ya kuzinduliwa zoezi hilo.Mwenyekiti Beda ni moja ya viongozi wa CCM waliohesabiwa 23 Agosti 2022.


Picha3:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko alipokutana na Wafanyabiashara wa Soko kuu Manispaa ya Mpanda na kuwapa elimu ya Sensa saa chache baada ya kuanza kwa zeoezi hilo 23 Agosti 2022.



Picha 4:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko alipotembelea moja ya Wakazi wa Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda kujiridhisha na utekelezaji wa zoezi la Sensa ya watu na makazi 23 Agosti 2022.



Picha5:Karani wa Sensa akitekeleza majukumu yake katika moja ya Kaya ndani ya  Manispaa ya Mpanda ikiwa ni saa chache baada ya kuzinduliwa  zoezi la Sensa 23 Agost 2022.



Picha 5:Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.Jamila Yusuph Kimaro akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Redio ya Kijamii Mpanda FM Bw.Betroid Chove wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa zoezi hilo ikiwa ni saa chache tangu kuzinduliwa kwake 23 Agosti 2022.Vyombo vya Habari vimeshiriki kwa sehemu kubwa katika kutoa Elimu ya  Sensa ya watu na makazi 2022.


Picha 6:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Redio ya Kijamii Mpanda FM Bw.Betroid Chove wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa zoezi la Sensa ya watu na makazi katika Manispaa ya Mpanda ikiwa ni saa chache tangu kuanza kwa zoezi hilo.Vyombo vya Habari vinashiriki kwa sehemu kubwa katika kufikisha Habari kuhusu Mwenendo mzima wa zoezi la Sensa ya watu na makazi 2022.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • RC MRINDOKO AZINDUA MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA NA MAZAO MENGINE KWA MWAKA 2025/26

    June 09, 2025
  • RC MRINDOKO AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA KATAVI, ATOA WITO WA AMANI NA USHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025.

    June 05, 2025
  • JAJI MKUU WA TANZANIA ASISITIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA UTOAJI HAKI.

    May 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.