Wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF awamu ya awamu ya tatu kipindi cha pili mkoani Katavi wameendelea kujivunia mafanikio kwa kuonyesha namna ambavyo kiasi kidogo cha fedha wanachokipata kimefanikisha kubadili maisha yao.
Ni usuhuda ambao wameutoa katika kikao cha tathimini ya utekelezaji katika eneo la utendaji wa mpango huo kilichofanyika leo Juni 27, 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambapo wamesema mbali na kupatiwa pesa taslim wamepatiwa maarifa ambayo yamebadili maisha yao.
"kabla ya mpango huu nilikuwa katika mazingira hatarishi yaliyojaa umasiki na sikuweza kuihudumia familia yangu hata kwa mlo mmoja wa uhakika, kwa sasa nimaweza kubadili milo hadi kufikia milo mitatu kwa siku, ninasomesha watoto, ninamifugo na ninaendesha kilimo cha kisasa kutokana na elimu ya kilimo cha kisasa ambayo nilipatiwa na wawezeshaji," amesema Hamisa Selemani mnufaika wa Tasaf.
Aidha Veronika Kipeta ambaye ni mnufaika tangu 2021 amesema kutokana na kiasi kidogo anachokipata kimemuwezesha kupata mtaji na hivyo anaendesha biashara ndogo ambayo inamnufaisha kiasi cha kumudu gharama za kusomesha watoto na hadi kufikia ngazi ya elimu ya juu ambapo watoto hao pia ni wanufaika na serikali imewapatia mkopo wa elimu ya juu kwa 100%
Kuelekea kumalizika kwa mradi huu wa Tasaf awamu ya tatu kipindi cha pili Afisa uwezeshaji na ufatiliaji kutoka Tasaf amesema wanufaika wamejengwa kwenye vikundi ambavyo viliwawezesha kupata ujuzi ambao utawawezesha kujisimamia kiuchumi kwa kusaidizana na wataalam walipo katika halmashauri.
Awali akifungua kikao hicho katibu tawala mkoa wa Katavi, Albert Msovela amewata wataalam katika halmashauri za wilaya kuendelea kuwasimamia kwa kuwapa elimu stahiki ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea mazingira wezeshi ili shughuli za kiuchumi wanazozifanya zikawe na tija.
Amesema kutokana na ushuhuda uliotolewa na wanufaika wa mpango wa Tasaf ni wazi kwamba wataalamu wakiendelea kuwasimamia watajijenga zaidi kiuchumi kwani mpango huo unapokamilika haina maana ya kuwa shughuli za kiuchumi na uzalishaji zitasimama bali ni mwanzo wa wao kuonyesha namna ambavyo wanaweza kujisimamia kiuchumi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi
Telephone: 025-2957108
Mobile:
Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.