• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Wanne wasimamishwa kupisha Uchunguzi, Matumizi ya Milioni 300 Ujenzi Hospitali Nsimbo,

Posted on: September 17th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mhe. Mwanamvua Mrindoko, ameagiza kusimamishwa kazi watumishi wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, kupisha uchunguzi wa   utata wa matumizi ya Sh milioni 300 za ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo.

Maagizo hayo ameyatoa 17 Septemba 2022 mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo, ambapo baada ya kupokea Taarifa ya Matumizi ya fedha za Ujenzi wa Hospitali hiyo alibaini utata katika matumizi ya Shilingi Milioni 300.

Waliosimamishwa kazi ni  pamoja na Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkuu wa Idara ya Afya, Ofisa Mipango pamoja na mkaguzi wa ndani kwa kumdanganya kuhusu matumizi ya fedha hizo.

Pia amemuelekeza mkaguzi wa ndani wa Mkoa, pamoja wataalam wengine waliopo chini ya Katibu Tawala wa Mkoa, ndani ya siku saba kukagua Sh milioni 300, namna zilivyotumika, huku akitoa siku nyingine 30 kukagua miradi yote inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo, ikiwemo vituo vya afya, shule na vituo vya tozo.

“Hii inaanza kunipa wasiwasi kwamba inawezekana hata hiyo miradi mingine kuna mambo ambayo hayaendi vizuri,” amesema RC Mrindoko.

Ameiagiza TAKUKURU Mkoa wa Katavi kukagua kwa undani mradi mzima wa hospitali ya Wilaya Nsimbo, ili kubaini ubadhirifu uliofanyika kuanzia matumizi ya fedha, ubora wa mradi, ununuzi wa vifaa na thamani zake na endapo watabaini wabadhirifu hatua kali za kisheria zichukuliwe.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf alimwambia mkuu wa Mkoa kuwa, Kamati ya Usalama Wilaya, baada ya kufuatilia matumizi ya Sh milioni 300, waliambiwa kiasi cha sh mil 210 zimetumika katika matumizi mengine nje na eneo lililokusudiwa, hivyo wakamuagiza mkurugenzi kufuatilia fedha hizo zilitumika vipi, lakini hakupata majibu.

“Hii milango unayoiona yote ilikataliwa na aliyekuwa Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu, hata kuridhia shilingi milioni 300 itoke kwa ajili ya kufanya umaliziaji ni pamoja na kutengeneza milango, ambayo unaiona hadi leo bado ipo, mimi ninachojua hiyo fedha haikutumika,” alisema DC Jamila.

Hata hivyo imeonekana katika ukaguzi wa ujenzi wa mradi huo, kwa nyakati mbalimbali baina ya Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mganga Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Mkoa wote walipokea taarifa zisizofanana.

“Sisi tulivyokuja na kamati yako iliyokuja kukuwakilisha, maelezo tuliyopewa na uliyopewa wewe leo ni tofauti kabisa, sasa sielewi aliyedanganywa kati yetu ni nani, lakini nadhani umedanganywa wewe mheshimiwa Mkuu wa Mkoa,”alisema DC Jamila

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • RATIBA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI - MWAKA 2025 April 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOA WA KATAVI August 27, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOA WA KATAVI August 27, 2025
  • View All

Latest News

  • RC MRINDOKO AKAGUA MIRADI YA MAJI MPANDA, ATOA MAAGIZO YA KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI.

    September 03, 2025
  • RC MRINDOKO AHIMIZA AMANI NA USHIRIKIANO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025.

    September 01, 2025
  • MFUMO WA E - MABORESHO KUIMARISHA UTENDAJI KWA WATUMISHI WA UMMA.

    August 26, 2025
  • MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA YAFIKIA TAMATI, DC BUSWELU AWASISITIZA UZALENDO

    August 26, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.